Home KITAIFA TANESCO kuwaunganisha wateja umeme ndani ya siku moja

TANESCO kuwaunganisha wateja umeme ndani ya siku moja

📌Ni katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa Wateja yanayofanyika katika viwanja vya Mwembe yanga.

📌RC Chalamila kuzindua utekelezaji mpango wa kuwakopesha majiko ya umeme wateja wapya watakaounganishiwa umeme na kulipa kupitia manunuzi ya umeme

Na Josephine Maxime, Dar es saaam

KATIKA kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, TANESCO imekuja na program maalumu ya kuwahudumia wateja wao Kwa kuwaunganishia wateja wapya huduma ya umeme ndani ya siku moja, ikiwa ni sehemu ya kusogeza huduma karibu na wateja wao.

Akizungumza katika maadhimisho hayo yanayofanyika katika viwanja vya mwembe yanga jijini Dar es salaam, Irene Gowelle ameeleza kuwa TANESCO imekuja na program hiyo ya TANESCO Mtaani kwako kwa lengo la kuwahudumia wananchi wa mkoa wa Dar es salaam ambapo wafanyakazi muhimu wa vitengo mbalimbali vya shirika wameweka kambi kwenye viwaja hivyo kwa siku tatu kuanzia leo Oktoba 08 ili kutoa huduma kwa wananchi.

Vilevile amesema kwa siku ya alhamisi wanatarajia kuwa na hafla ya uzinduzi wa mpango maalum wa kuwaunganishia umeme wateja wapya na kuwakopesha majiko ya umeme kwa wale watakaopenda kutumia nishati ya umeme kwenye kupika na kwamba watayalipa kidogo kidogo kupitia manunuzi yao ya umeme kwa mkataba wa miezi sita hadi mwaka mmoja.

Mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya mradi wa Shirika unaofadhiliwa na Taasisi ya Mecs ambao umedhamini majiko ya umeme mapya elfu moja kwa majaribio ya awali ya mpango huo.

‘’ TANESCO tumeona tuadhimishe wiki ya huduma kwa mteja kwa kusogeza huduma kwa jamii, tumekuja na program ya TANESCO Mtaani kwako kwa lengo la kuwahudumia wananchi wa mkoa wa Dar es salaam, ni fursa ya pekee kwa wananchi kufika katika viwanja hivi vya mwembe yanga kupata elimu na mambo mbalimbali yahusuyo Shirika,’’amesisitiza Gowelle.

Aidha, amebainisha kuwa wananchi watapata fursa ya kushuhudia maandalizi ya vyakula mbalimbali kwa kutumia majiko yanayotumia umeme kidogo pamoja na kupata elimu kuhusu matumizi bora ya umeme,usalama ,ulinzi wa miundombinu na operesheni inayoendelea ya ukaguzi wa mita

Gowelle pia amewakaribisha wananchi kushiriki katika uzinduzi rasmi utakaofanyika Oktoba 09. 2025 katika viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam, ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.

Maadhimisho haya yanafanyika chini ya kaulimbiu isemayo: “Mpango Umewezekana”, ikilenga kuonesha mafanikio ya huduma za TANESCO na dhamira ya Shirika hilo katika kuwahudumia Watanzania kwa haraka, ufanisi na ubunifu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here