Home SIASA Gombo aahidi kununua meli kubwa ya kisasa

Gombo aahidi kununua meli kubwa ya kisasa

Na Mwandishi wetu, Ruvuma

MGOMBEA Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito Gombo, amesema atakapopata ridhaa ya kuwa Rais kwenye Serikali yake atanunua meli kubwa na ya kisasa ambayo itawaunganisha wafanyabiashara wa Malawi na Tanzania kupitia ziwa nyasa.

Mgombea urais huyo ametoa kauli hiyo wakati akiwa kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika Wilaya ya Songea mjini Viwanja vya soko kuu la Songea Mkoani Ruvuma ambapo ameleeza umuhimu wa reli hiyo pamoja na meli ya kisasa kuwa vitakuwa kichocheo cha mapato na ukuaji uchumi katika Mkoa huo.

Amesema ili kuhakikisha anaufungua mkoa wa Ruvuma atajenga reli mpya ya kisasa kutoka Mkoani Mtwara mpaka Mbamba bay itakayorahisisha wafanyabiashara wa malawi kuchukua mizigo yao bandari ya Mtwara badala ya Dar es salam ili kupunguza umbali na msongamano.

“Kutakuwa na reli nyingine ya kisasa kutoka Mtwara kwenda Mbambabay na kutoka Mbambabay kwenda Catabey Serikali ya chama cha wananchi CUF kitajenga meli kubwa pale ili mizigo inayotoka Mtwara kwenda Malawi itapitishwa pale bandari ambayo itakwenda Mbambabay tunajenga,”amesisitiza Gombo.

“Lakini reli hiyo hiyo tutaitoa Songea kwenda Tabora mpaka Mwanza tutaijenga na itapita kule kwenye madini ya chuma kwahiyo tutajenga kwasababu pesa zipo na maliasili zote zipo ndugu zangu niwaombe sana sana tarehe 29 mkanichague mimi Gombo Samandito Gombo,”amesema.

Pia amewataka watanzania kujitokeza terehe 29 kwenda kupiga kura na badala yake amewataka wawapuuze wale wote wanaojaribu kutaka kususia uchaguzi.

“Niwaombe sana ndugu zangu tarehe 29 msifanye makosa ya kwenda kuandamana na kuacha kwenda kwenye uchaguzi hiyo ni janja ya CCM ya kuwafanya mkienda kuandamana hampigi kura na wao wanatatangazwa washindi, watu Zanzibar walisusia uchaguzi ccm wakajipa ushindi sisi tukapige kura tukimaliza turudi tukalinde kura zetu,”amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here