Home SIASA Gombo: Nikiwa rais kuunda tume ya kuchunguza utekaji na mauaji watu

Gombo: Nikiwa rais kuunda tume ya kuchunguza utekaji na mauaji watu

Na Mwandishi wetu, Mbeya

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito Gombo amesema atakapoapishwa kuwa rais ataunda tume ya kuchunguza matukio ya utekaji na mauaji ya watu waliofariki na waliopotea.

Mgombea urais Gombo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la Uyole Mkoani Mbeya ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake za kunadi sera na ilani za chama chake amesema matukio hayo yamekuwa yakitokea huku wahusika wakiwa hawajulikani wakijinasibisha na polisi.

Amesema atakapopata ridhaa ya kuwa Amiri jeshi mkuu kwenye Serikali yake ataunda tume kwa haraka ya kuchunguza upotevu wa watu ambao umekuwa ukitokea huku wahusika wakiwa hawuchaguzi2025

“Watanzania milioni 70 tunaishi kwa wasiwasi kwasababu ya watu wachache wanaojiita wasiojulikana na sisi tumekubali kwa wingi wetu wote huu kweli lugha ya watu wasiojulikana Tanzania iwe lugha sasa ya kuongelea tumekaa tumetulia na tumekubali kwa wingi wetu huu vijana mpo na mmetulia tu,”amesema Gombo.

“Nchi hii itajengwa na kulindwa na vijana haiwezi kujengwa na kulindwa na wazee, wazee wameshamaliza kazi yao nyinyi vijana mnakubali watu wachache wanaijiuta wasiojulikana wanakuja kuteka watu kisa wanajiita wao ni polisi au ni vyombo vya dola na kwasababu polisi saa nyingine huwa wanakamata watu wakiwa hawana uniform na bunduki wanazo na hawa wanaojiita wasiojulikana na wenyewe wanakamata watu wakiwa na bunduki wanajinasibisha na polisi na wenyewe hawana uniform sisi wananchi tunashindwa kutofautisha kati ya jambazi ni nani na polisi ni nanikwahiyo kama tunashindwa kuwatofautisha hawa watu tusikubali kuwa wanyonge tusipelekwe kama Ng’ombe au kama nyumbu porini,”amesisitiza Gombo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here