Home KITAIFA Chalamila amkabidhi Mjane Alice hati yake

Chalamila amkabidhi Mjane Alice hati yake

Na Esther Mnyika, Dar es Salaam

MKUU  wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert  Chalamila amemkabidhi hati ya nyumba mjane wa marehemu Justus Rugaibula, Alice Haule, iliyopo katika eneo la Msasani Beach, baada ya tume iliyoundwa kuchunguza na kupitia malalamiko kuhusu  mgogoro  wa nyumba na Mohamed Mustafa  kumalizika  na kumkabidhi shilingi milioni 10.

Pia ametoa siku tano kwa Mohamed Mustafa kujisalimisha kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa au kwa Jeshi la Polisi kabla hatua zaidi hazijachukuliwa.

Akizungumza leo Oktoba, 20 2025 jijini Dar es Salaam amesema amemkabidhi mjane huyo hati hiyo ya kiwanja Namba 819, kama msimamizi wa mirathi ya marehemu mume wake Justus Rugaibula.

 Amesema  hivi karibuni Alice alipitia Changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya Kudhalilishwa kwa kutaka kuondolewa kwa nguvu ndani ya nyumba hiyo na Mohamed Mustafa mara baada ya video zake kuenea kwenye mitandaoni ya kijamii.

Amedai  Mustafa amekuwa na maelezo yasiyoeleweka katika maelezo yake huku akiviagiza vyombo vya dola kuendelea kumtafuta Mohamed mbali na kadhia hiyo pia anadaiwa kutumia majina ya viongozi katika maelezo yake kwa kujinasibu amekuwa rafiki wa karibu na viongozi.

“Namtaka Mohamed Mustafa Yusufali kujisalimisha katika jeshi la polisi kufuatia shutuma zinazomkabili za kujipatia nyumba ya mjane wa marehemu Justus Rugaibula ,Alice Haule iliyopo Msasani Msasani Beach kiwanja Na.819 kinyume cha sheria,”amesema.

Wakati huohuo akizungumzia hali ya usalama katika mkoa wa Dar es Salaam ni shwari hasa  kuelekea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Amesema jana wamepata ratiba ya Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk.Samia Suluhu Hassan atakuwa Dar es Salaam kuanzia Oktoba 21 hadi 23 kwa kufanya mikutano mitatu ambapo atakuwa na mkutano utakafanyika viwanja vya Leaders ,uwanja wa Kinyerezi na viwanja vya Tanesco vilivyopo Temeke.

Amewahakikishia  wanaCCM  na watanzania kwa ujumla mgombea huyo atanadi sera zake katika mkoa wa Dar es Salaam na kuondoka salma bila kuingilia na kitu chochote kama ilivyofanyika kwa wagombea wengine wa siasa kwahiyo niwaase watanzania kuendelea kuwa wasikivu na ushirikiano wa kutosha bila kujali ukubwa au udogo wa chama huku sote wakiwa na dhana wanajenga nchi moja kwa maslahi mapana na maendeleo ya watanzania.

“Nitoe rai kwa watanzania kwenda kujitokeza kwa wingi katika kushiriki haki ya msingi ya kidemokrasia hali mkijua demokrasia ni moja ya kiashiria cha utawala bora hivyo wajitokeze kwenda kuchagua viongozi wanaowahitaji na kushiriki mchakato huoa mbalo ni takwa la kisheria liliandikwa katika katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake”amesema

Naye Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam Shukuru Kyando amesema baada ya kupokea maoni kutoka kwenye timu iliyoundwa kufanya uchunguzi wameamua kuwa haki ya umiliki wa nyumba urudishwe kwa Alice Haule ambaye ndio msimamizi wa mirathi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hati hiyo Alice Haule alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan  kwa kuwajali wanyonge na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila na Jeshi la polisi na Vyombop vya habari kupaza sauti na hatimaye kuweza kupata haki yake.

Mjane Alice Haule alivamiwa na kuondolewa nyumbani kwake kwa nguvu na Mohamed Yusufali ambapo inadaiwa alinunua nyumba hiyo iliyopo mikocheni Dar es Salaam kutoka kwa marehemu Justice Rugaibula kabla ya kifo chake mwaka 2011.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here