Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Samia Suluhu Hassan amesema upatikanaji wa umeme jijini Dar es salaam ni mkubwa kutokana na Miundombinu wezeshi ambayo inatekelezwa na serikali ya awamu ya sita hivyo huduma ya umeme inapatikana Masaa 24.

Akizungumza Oktoba 21 2025 Jijini Dar e salam Dk. Samia na Wananchi wakati wa Wa muendelezo wa kampeni kwenye mkoa huo amesema huduma ya umeme mkoani dar es salam imeimarika kwa kiasi kikubwa kutokana na uwekezaji wa serikali ya Awamu ya sita.
Amesema kipindi cha nyuma tulikuwa na changamoto ya umeme ambayo ilipelekea kuwepo kwa mgao huo wa umeme kwenye baadhi ya Maeneo.
“Sasa hivi umeme ni saa 24 ukikosekana kwa dakika chache kunakuwa na Taarifa rasmi kutoka kwenye Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa nini umeme umezimwa kuna sababu y kukosekana kwa huduma ya umeme kwa muda kadhaa,”ameeleza.