
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia CCM, Paul Makonda akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara na wananchi katika soko la Darajani, Zanzibar huku akionesha mfano wa karatasi ya kupigia kura akihamasisha wananchi kupiga kura kwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na mgombea mwenza wake Dk. Emmanuel Nchimbi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Katika hatua nyengine Paul Makonda alipata nafasi ya kusalimiana na mmoja wa wananchi wa Zanzibar alipowasili katika soko la Darajani kuendelea na kampeni za uhamasishaji wa wapiga kura kumuunga mkono mgombea urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Pembeni ni baadhi ya wananchi waliokusanyika kushuhudia tukio hilo.


Aidha Makonda alimwonesha mwananchi mfano wa karatasi ya kupigia kura iliyoandaliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, akielezea namna ya kutiki kwa usahihi jina la mgombea urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.



