Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limetoa Onyo kali kwa Mashabiki wote wa Klabu ya Simba na Yanga kutoingia na kifaa chochote cha silaha katika Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Mechi ya Oktoba 25 na 26 Mwaka huu.

Onyo hilo amelitoa Leo Oktoba 24,2025 Jijini Dar es salaam Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema Jesh wiki hii kutakuwa na michezo ya soka ya kimataifa ya timu zote mbili za Tanzania ambapo mtanange wa kwanza ni Oktoba 25,2025 saa 11.00 jioni timu ya Yanga ya Tanzania itacheza na Silver Strikers ya Malawi.
Pia Oktoba Oktoba26,2025 saa 10:00 jioni Simba itacheza na Nsingizini ya Eswatini hivyo Jeshi limejiandaa vizuri kuimarisha Ulinzi na Usalama katika eneo la Uwanja wa Benjamini Mkapa
” Nawakumbusha Mashabiki na wapenzi wote wa soka kuwa silaha ya aina yoyote haitaruhusiwa uwanjani, Vitendo vyovyote vya vurugu au kuashira uvunjifu wa amani au vilivyo kinyume na sheria pia havitavumiliwa” amesisitiza.
Amesema kumekuwa na Mashabiki Kutumia lugha chafu za Matusi Wakati kuna Viongozi, watu wenye heshima zao wanahudhuria hivyo siku hiyo amewaomba midomo yao wakithubutu tu watashughulikiwa kisheria mara moja .
Aidha Jeshi la Polisi wanatoa wito kwa wadau wote wa soka kufuata taratibu za kuingia uwanjani Magari yasiyo na kadi za kuingia uwanjani hayataruhusiwa



