Home KITAIFA Niffer na wenzake 21 wamesomewa mashtaka matatu ikiwemo uhaini

Niffer na wenzake 21 wamesomewa mashtaka matatu ikiwemo uhaini

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

MFANYABIASHARA Jenifer Jovin (26) maarufu Niffer na wenzake 21 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa kesi uhaini.

Niffer na wenzake hao wamefikishwa Mahakamani hapo leo mchana, Ijumaa Novemba 7, 2025 na kusomewa mashtaka matatu, ambayo ni kula njama ya kutenda kosa la kuharibu miundombinu na mawili ni ya uhaini.

Kosa la kwanza linalowahusu washtakiwa wote 22 ambapo ni kwamba kwa pamoja wamekula njama ya kutenda kosa au kupanga uhalifu ambao ni uhaini

Kosa la pili ambalo ni la uhaini linawahusu washtakiwa 21 isipokuwa mshtakiwa mmoja pekee ambaye ni Niffer, ambapo washtakiwa walianzisha nia ya kuzuia uchaguzi Mkuu 2025, na kutishia mamlaka na wakatekeleza nia hiyo kwa kufanya vurugu zilisababisha uharibifu wa mali za umma,

Na kosa la tatu la uhaini pia linamuhusu mshtakiwa namba moja pekee ambaye ni Niffer, ambapo alihamasisha watu kuvuruga uchaguzi Mkuu 2025 na kuhamasisha umma kununua barakoa za kuzuia mabomu ya machozi kutoka dukani kwake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here