Home KITAIFA Serikali yaunda Tume maalumu kuchunguza ghasia za Oktoba 29 — Rais Samia

Serikali yaunda Tume maalumu kuchunguza ghasia za Oktoba 29 — Rais Samia

Na Esther Mnyika, Dodoma

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewaongoza Wabunge wa Bunge la Tanzania na wageni waalikwa kusimama na kuomba kwa dakika moja kwaajili ya Wananchi waliopoteza maisha kwenye vurugu na ghasia za Jumatano ya Oktoba 29, 2025 katika Miji ya Arusha, Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Songwe.

Pia ametoa pole kwa waliofariki, kujeruhiwa na kupoteza mali na amesema Serikali imeunda Tume ya kuchunguza yaliyotokea.

Rais Dk. Samia ameongoza jambo hilo leo Ijumaa Novemba 14, 2025 Bungeni jijini Dodoma wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge la 13 la Tanzania akitangaza pia kuunda Tume maalumu ya kuchunguza tukio hilo, akitoa pole pia kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao.

“Mimi binfasi nimehuzunishwa sana na tukio lile natoa pole kwa Familia zote zilizopoteza Familia zao tunaomba waliofariki wapumzishwe kwa amani, kwa majeruhi tunawaombea wapone haraka na waliopoteza mali zao tunawaomba wawe na ustahimilivu,” amesema.

Amesema Serikali imechukua hatua ya kuunda Tume ya kuchunguza yaliyotokea ili tujue kiini cha tatizo, taarifa hiyo itatuongoza kujielekeza kwenye mazungumzo ya kuleta maelewano na amani.

Pia Rais Dk. Samia amvielekeza Vyombo vya Ulinzi na Usalama hususani Ofisi ya DPP kuchuja makosa ya Vijana walioshtakiwa kwa makosa ya uhaini kufuatia maandamano ya Oktoba 29,2025 na kwa wale waliofanya makosa kwa kufuata mkumbo waachiwe huru.

Amesema kuwa kwa wanangu wa Taifa hili la Tanzania sisi wazazi wenu kama wangefanya hayo mliofanya leo nchi isingefika hapa wala maendeleo wanayoona leo.

“Natambua kuna Vijana wengi wamekamatwa kwa kushtakiwa kwa makosa ya uhaini hawakujua wanachokifanya na wengine wamefuata mkumbo, nikiwa kama Mama navielekeza vyombo vya kisheria kuangalia makosa yaliyofanywa na Vijana wetu, kwa wale ambao walifanya mambo kwa kufuata mkumbo na hawakudhamiria kufanya uhalifu wawafutie makosa yao.

Ukiangalia clip zile za maandamano unaona kabisa kuna Vijana waliingia kwa kufuta mkumbo, wanaimba kwa ushabiki, naelekeza Ofisi ya DPP kuchuja viwango vya makosa na kwa waliofuata mkumbo wawaachie waende kwa Wazazi wao,”amesema

Amesisitiza kuwa vijana wa Tanzania Nchi hii ni yenu kwa shida zozote zile zinazowakabili wasikubali hata siku moja kushawishiwa kuichoma Nchi yenu wenyewe wasikubali kukata tawi la mti ambalo mmeukalia wsikubali kabisa hili nawaomba walikatae kwa nguvu zenu zote ninyi ndio walinzi na wajenzi wa Taifa hili nawasihi kamwe wasije kuwa wabomoaji wa Taifa lenu.

“Kuna wakati vijana mnafuata mkumbo wa uhalifu kwa ushabiki, ninatambua kwamba vijana wengi waliokamatwa na kushitakiwa kwa makosa ya uhaini hawakujua wanachokifanya, nikiwa mama na mlezi wa Taifa hili ninavielekeza Vyombo vya Sheria na hasa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kuangalia kiwango cha makosa yaliyofanywa,”amesema.

Rais Dk. Samia amesema yeye na wenzangu Serikali wamefikiria kuwa na Wizara kamili itakayoshughulikia mambo ya Vijana, wameamua kuwa na Wizara kamili badala ya kuwa na Idara iliyo na mambo mengi, vilevile nafikiria kuwa na Washauri wa mausala ya Vijana ndani ya Ofisi ya Rais.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here