Home KITAIFA Wahamiaji haramu 14 wakamatwa mwanza

Wahamiaji haramu 14 wakamatwa mwanza

Na Mwandishi wetu, Mwanza

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia wahamiaji haramu 14 raia wa Burundi waliokamatwa wakiwa wameingia nchini kinyume na sheria, kwa kutumia magari mawili tofauti ya abiria.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, Novemba,23 2025 wilayani Sengerema, wakati akizungumza na umma kupitia vyombo vya habari .

Amesema mafanikio hayo yametokana na ufuatiliaji wa mienendo ya kihalifu pamoja na uwekaji wa vizuizi barabarani .

Ameeleza kuwa katika Kijiji cha Busisi, Tarafa ya Sengerema, wahamiaji haramu 13 walikamatwa Novemba 23, 2025 majira ya saa 7:30 mchana wakiwa wanasafiri ndani ya gari aina ya Tata lenye namba za usajili T 337 DYA, mali ya Chiza Francis Lugubi, mkazi wa Dodoma, ambalo husafiri kati ya Kabanga (Ngara, Kagera) na Mwanza.

Wakati wa kukamatwa, dereva wa gari hilo, aliyetambulika kwa jina la Jonas Richard, alitoroka na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika usafirishaji wa wahamiaji hao ni Mustahper Emily (24), fundi magari na mkazi wa Kahama, Shinyanga, pamoja na Pendo Matembere (36), kondakta na mkazi wa Nyegezi, Mwanza.

Baada ya mahojiano, ilibainika kuwa wahamiaji hao waliingia nchini kupitia mpaka wa Kabanga mkoani Kagera mnamo Novemba 22, 2025.

Mtuhumiwa wa 14, Shadia Japhari Majaliwa (18), raia wa Burundi na mkazi wa Kisuru, alikamatwa katika eneo la Nyatukala wilayani Sengerema akiwa ndani ya gari aina ya Yutong lenye usajili T 131 DRE.

Magari yote mawili yanashikiliwa na jeshi la Polisi huku dereva na wasaidizi wengine wakiendelea kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za kuwasafirisha wahamiaji haramu.

Akitaja majina ya wahamiaji waliokamatwa ni:-

  1. Nkurunzinza Eloi (38), Mhuhutu, Muyinga
  2. Bizimana Aster (20), Mhuhutu, Muyebe
  3. Tanishaga Renova (20), Mhuhutu, Muyebe
  4. Nyosaba Anatory (23), Mhuhutu, Muyebe
  5. Niyokuru Jlock (23), Mhuhutu, Muyebe
  6. Nsolimana Evariste (30), Mhuhutu, Ngozi
  7. Riyazimana Jerome (30), Mhuhutu, Ngozi
  8. Mbonipa Claude (23), Mhuhutu, Ngozi
  9. Ntirampera Oleste (42), Mhuhutu, Nyanzalaki
  10. Mbalishimana Swalidi (47), Mhuhutu, Kitega
  11. Sindobizero Osca (28), Mhuhutu, Tangala
  12. Irakize Derise (27), Mhuhutu, Ngozi
  13. Elias Sinilemeya (31), Mhuhutu, Kitega
  14. Shadia Jafhari (18), Mrundi, Kisuru

Kamanda Mutafungwa amesema Jeshi la Polisi litaendelea kuimarisha doria na vizuizi barabarani kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama pamoja na wananchi ili kudhibiti matukio ya kihalifu. Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa zitakazosaidia kuwafichua wahalifu kabla hawajatekeleza uhalifu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here