
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Isack Kihwili (wa tatu kutoka kushoto) akishiriki katika kikao jijini Lisbon, Ureno ambako unafanyika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Kimataifa ya Taasisi za Bima ya Amana (IADI-AGM). Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma na Itifaki wa DIB, Lwaga Mwambande. Mikutano ya IADI ambayo ilianza tarehe 24 Novemba, inatarajiwa kuhitimishwa Novemba,28 2025.
Mapema katika Mkutano wa Kamati ya Kanda ya Afrika (ARC), pamoja na mambo mengine, ilipokea taarifa ya Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kuanza kutekeleza jukumu la kupunguza hasara kwa benki au taasisi ya fedha inayopitia changamoto.

Jukumu hili limeanza rasmi kutekelezwa na DIB Julai 2025. Lengo ni kuhakikisha benki au taasisi ya fedha inayopitia changamoto katika biashara yake kusaidiwa ili irudi katika hali ya kawaida badala ya kusubiri hadi benki au taasisi hiyo ya fedha ife na kulipa fidia. Kupunguza hasara kunaweza kuwa nafuu zaidi kuliko kama taasisi kama hiyo ikaachwa hadi ianguke.



