Home KITAIFA FCC kuongeza uelewa kuhusu athari za teknolojia ya AI

FCC kuongeza uelewa kuhusu athari za teknolojia ya AI

Na Esther Mnyika, Dar es Salaam

TUME ya Ushindani FCC) imeanza maadhimisho ya wiki ya ushindani Ikiwa lengo la kuongeza uelewa kwa umma kuhusu athari za teknolojia ya akili mnembe(AI) katika ushindina wa masoko na maadhimisho hayo yanahimiza utekelezaji wa serana sheria za ushindani katika kukuza uchumi.

Pia Tume inaungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha Siku ya Ushindani Duniani ifikapo tarehe 5 Desemba 2025, maadhimisho yanayofanyika kila mwaka kufuatia maazimio ya Umoja wa Mataifa tangu mwaka 1980.

Akizungumza leo Novemba, 1 2025 Jijini Dar es Salaam na waandishi wa habariKaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Khadija Ngasongwa,kuhusu maandalizi ya maadhimisho hayo yenye kaulimbiu isemayo “Akili Mnemba (AI), Walaji na Sera za Ushindani,”

“Akili Mnemba ni eneo linalokua kwa kasi, na FCC tunaangazia kwa umakini namna matumizi yake yanavyoathiri masoko, hususan masuala ya usalama wa taarifa, uvujaji wa siri za kibiashara na upendeleo unaotokana na ‘algorithimic bias’,” amesema.

Amesema shughuli hizo zitafanyika kuanzia Disemba 1 hadi Disemba 5, 2025, zikiwahusisha semina kwa mamlaka za udhibiti, mafunzo kwa wanasheria, utoaji elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari, pamoja na kongamano maalum la kitaifa.

“FCC tunaungana na dunia nzima kuadhimisha siku hii muhimu ambayo inalenga kuimarisha uelewa kuhusu umuhimu wa ushindani wenye afya katika masoko.Wiki ya maadhimisho itakuwa na matukio mbalimbali yenye lengo la kuelimisha na kuhamasisha wadau juu ya masuala ya ushindani na haki za walaji,” ameeleza.

Amesema chimbuko lake lilitokana na uamuzi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha kanuni za kudhibiti vitendo vinavyofifisha ushindani maarufu kama “The UN Set.”

“Kanuni hizi ndizo zimeweka misingi ya sera na sheria za ushindani duniani, na Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayoziongoza shughuli zake kwa mujibu wa mwongozo huo,” amesema.

Amesema Tanzania inaendelea kutekeleza sera na sheria hizo ili kuzuia ukiritimba, kulinda nguvu ya ushindani, na kuhakikisha masoko yanabaki huru na yenye tija kwa uchumi na jamii.

Katika kufafanua majukumu ya FCC, alisema Tume imekuwa ikidhibiti upangaji bei, matumizi mabaya ya nguvu ya soko, na miungano ya makampuni inayoweza kudhoofisha ushindani

“Kwa sasa, kampuni zenye mauzo au thamani ya kuanzia shilingi bilioni 3.5 ndizo zinazotakiwa kutuarifu zinapokusudia kuungana au kununuliana hisa,” amefafanua.

Akizungumzia kaulimbiu ya mwaka huu, Ngasongwa amesema imekuja wakati ambapo serikali inasisitiza kwa nguvu matumizi ya TEHAMA chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Hata hivyo, amesema teknolojia hiyo ikitumika vyema inaleta manufaa makubwa.

“AI inaleta ubunifu, inapunguza gharama za uendeshaji, inafungua masoko mapya ya kilimo, afya, elimu na fedha, na inaongeza ushindani wenye faida kwa jamii nzima, hususan vijana,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here