Na Esther Mnyika, Dar es Salaam
WIZARA ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekiri uwepo wa wanafunzi wanaoacha shule kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo zakifamilia na kueleza kuwa utafiti uliofanywa unaonesha mkoa wa Geita unaongoza kuwa na kundi hilo.

Pia ametangaza mabadiliko ya mtaala mpya wa elimu amesema kwa sasa wanaondokana na mtaala wa sasa wa ‘7+4+2+3+’ na kwenda kwenye mtaala mpya wa ‘6+4+2 au 3+3+’ ambao elimu ya msingi itaishia darasa la sita huku elimu ya sekondari kidato cha nne ikiwa ni ya lazima kwa watoto wote na sio hiyari kama ilivyo kwa mfumo huu wa sasa.
Akizungumza leo Disemba, 10 2025 na jijini Dar es Salaam Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema wanafunzi hufikia hatua hiyo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo suala la kifamilia huku kundi jingine likitoka katika mikoa yenye maeneo ya biashara.
Amesema kuwa Mtaala huo umeanza kufanya kazi kwa darasa la tatu wa sasa na wataishia darasa la sita mwaka 2027 ambapo watafanya mtihani wa majaribio utakao wawezesha kujiunga na kidato cha kwanza.
“Wanafunzi hufikia hatua hiyo kutokana na sababu mbalimbali zikiwe zakifamilia lakini wizara ilifanya utafiti umeonyesha kuwa kuwasuala la drop out(kuacha shule) si dogo hasa kwa mikoa
Geita inaongoza kwa sasa kwa sababu ya shughuli za madini,”amesema Profesa Mkenda.
Amesema pamoja na kufanya utafiti huo wizara kwa sasa imepanga mipango mbalimbali ikiwemo kuweka mfumo unganishi kwa wanafunzi ambao utakuwa ukifuatilia mwenendo wa mtu mmoja mmoja.
“Tunaweka mfumo unganishi wanafunzi wanapomaliza shule unapewa namba unafuatilia kila ulipo mfumo unafanyiwa kazi,kaa hiyo hata ukiacha shule mfumk unakufuatilia na kukufuata ulipo kutoa sababu ya kwa nini uliacha shule,”amesema.
Pia amegusia kuhusu ajira za walimu ambazo ziliahidiwa na Rais Dk.Samia Suluhu ambapo jumla ya walimu 7000 wanatarajiwa kunufaika.

“Ajira za elimu 7000 zitaanza kutolewa ndani ya siku 100 ambazo tayari zimeshatangazwa na watakapopatikana watapelekwa katika vituo vya kazi,”amesema Profesa Mkenda.
Amesema suala la elimu lazima litiliwe mkazo kwakuwa ili Nchi iendelee lazima uwekezaji mkubwa ufanyike katika maeneo muhimu hasa Sayansi, Teknolojia na ubunifu, ambapo amesema kwa kulitambua hilo Serikali imeweka msisitizo zaidi kwa Wanafunzi katika kusoma masomo hayo ya sayansi.
Amebainisha kwamba chini yaaelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kila Mkoa umejengewa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya sayansi huku mkakati ukiwa kujengwa nyingine za Wanaume.
“Kuna ’emphasize’ (msisitizo) kubwa sana imewekwa kwenye masomo ya sayansi, kwa mfano chini ya maelekezo ya Rais wetu kila Mkoa umejengewa Sekondari ya Wasichana ya sayansi” ameeleza.
Ameongeza kuwa ni maagizo ya Rais kuhakikisha Vijana wote wenye uwezo wa kusoma masomo ya Sayansi wanasomeshwa kwa gharama za Serikali, ili waendelee kusoma masomo hayo bila kuyaacha.
Aidha amesema kutambua kasi ya matumizi ya akili unde (Artificial intelligence) katika maeneo mbalimbali, ikiwemo usalama wa nchi, Kilimo na sekta nyingine za uchumi, Serikali imesema imeamua kuanza kufundisha maswala hayo, ili kuandaa wataalamu watakao hudumu katika eneo hilo.

“Eneo jingine kubwa ambalo kwa hakika dunia inaenda kwa kasi sana, eneo hili wanaita akili unde, yaani akili iliyoundwa, Artificial intelligence, mambo ya data Sayansi, na maeneo kama hayo, dunia inaenda kwa kasi sana hata maswala ya usalama wa nchi, uchumi, banking, kilimo, kinaenda kutegemea sana maswala ya akili unde,” amefafanua.
Amesema hadi sasa Vijana 50 wamechukuliwa na kupelekwa katika kambi ya mafunzo inayowaanda kwa kujifunza mambo mbalimbali, ili baadaye wapelekwe kwenda kusoma nje kwa utaratibu wa Serikali.
Aidha, amebainisha kuwa kundi la kwanza la Wanafunzi hao wataondoka mwisho wa Mwezi Januari kwenda Afrika Kusini kwajili ya masomo, huku kundi la Pili akisema litaondoka kwenda Ireland Mwezi wa 9, ambapo pia Wanafunzi hao.



