Home KIMATAIFA Balozi Kombo afanya ziara ya kikazi Washington D.C

Balozi Kombo afanya ziara ya kikazi Washington D.C

Na Mwandishi wetu, Marekani

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Mahmoud Thabit Kombo anafanya ziara Rasmi ya kikazi jijini Washington, D.C., nchini Marekani.

Katika ziara yake hiyo, Waziri Waziri atakukutana na wadau Mbali mbali muhimu katika kuimarisha uhusiano wa baina ya Tanzania na Marekani.

Wakati akiwa nchini Marekani, Waziri pamoja na masuala mengine, atakutana pia na kufanya mazungumzo ya kina na Serikali na Wabunge mbalimbali wa Bunge la Marekani.

Miongoni mwa viongozi ambao tayari amekutana nao ni Mbunge machachari wa Chama cha Republican, Brian J. Mast wa Jimbo la Florida, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Wawakilishi la Marekani na kukubaliana mambo kadhaa juu ya Uimarishaji mahusiano hayo na Tanzania pamoja na kupokea Mwaliko wa Kamati yake hiyo ya Bunge la Marekani kufanya ziara Rasmi nchini Tanzania mapema iwezekanavyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here