Home KIMATAIFA Urusi na Tanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta za mkakati

Urusi na Tanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta za mkakati

Na Mwandishi wetu, Misri

LEO Desemba, 19 2025, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Misri pembezoni mwa Mkutano wa Jukwaa la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Urusi na Nchi za Afrika, unaoendelea nchini Misri.

Nchi hizo pia zimekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta za kimkakati ikiwemo Elimu, Nishati, Afya, Kilimo, Miundombinu, Uchukuzi, na Utalii.

Pamoja na mahusano mazuri yanayoendelea kati ya Urusi na Tanzania, Waziri Kombo amemthibitishia Waziri Lavrov utayari wake katika kushirikiana na Serikali ya Urusi katika kuwezesha na kufanikisha utekelezaji wa miradi na masuala mbalimbali ya ushirikiano.

Aidha, kwa upande wake Waziri Lavrov ameahidi kuipatia Tanzania ushirikiano utakaohitajika katika maeneo yanayokusudiwa ili kuendelea kudumisha uhusiano wa kihistoria wenye maslahi mapana baina ya Tanzania na Urusi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here