Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
MCHUNGAJI wa Kanisa Christian Assembly, Daudi Mashimo ametoa wito maalum kwa viongozi wa dini wa madhehebu yote kusimama pamoja ili kuleta amani ya nchini.

Pia amesema Viongozi wa dini Waislamu na wakristo wawe pamoja katika kurudishi Taifa kuwa pamoja na kuwa wavumilivu kipindi hiki wakati Tume ya Uchunguzi Oktoba, 29 2025 inafanya kazi.
Akizungumza leo Disemba, 23 2025 Jijini Dar es salaam Mchungaji Mashimo mapema leo wakati a ametoa pole na faraja kwa ndugu na jamaa wote waliopoteza wapendwa wao, akisisitiza kuwa Taifa limepitia mapito mengi yanayohitaji mshikamano na subira.
“Kipindi hiki tuwa wavumilivu huku makanisa na madhehebu yote tulinde amani hakuna serikali iliyo kamilika duniani naomba tuwe na subra na hakuna asiyejua kilichotekea Oktoba, 29 2025 tuwe na subira wakati Tume inafanya kazi kwa kilichotokea,”amesema Mashimo.
Amesema Katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Christmas viongozi wa dini kutoka madhehebu yote wanapaswa kuwa kitu kimoja ili kuhakikisha Taifa linapata faraja, amani na utulivu, badala ya kutumia maumivu ya wananchi kama nyenzo ya kuchochea migawanyiko
“Tunapokwenda kusherekea sikukuu, naomba viongozi wa dini tuwe pamoja, siyo kipindi cha Watanzania kutupiwa mizigo ya kuwaumiza,” amesema.Viongozi wadini kusimamia kwa pamoja kuleta amani nchini
Mchungaji Mashimo amesema hakuna Serikali yoyote duniani iliyokamilika, hivyo mshikamano wa kitaifa ni muhimu wakati wote.
Amesema kuwa Sikukuu ya Krismasi inapaswa kuwa chombo cha kuwaunganisha Watanzania ili wawe kitu kimoja na kujenga Taifa lenye upendo na uvumilivu.
“Nipo upande wa Mungu ambaye yupo katika dhamana ya nchi hii, akiongeza kuwa maumivu yaliyopo yasigeuzwe fimbo ya kukumbushana matatizo, bali yawe msingi wa kujenga na kuimarisha Taifa,”amesema.
Aidha amewatakia Watanzania Krismasi njema, akisema ni maombi yake Yesu Kristo azaliwe upya katika mioyo ya watu wote.



