Na Mwandishi wetu,Dodoma.
TANZIA Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Mbogo Alexander Munubi, amefariki dunia ghafla Desemba, 28 2025, mkoani Dodoma.

Taarifa rasmi kutoka ofisini hapo imeeleza kuwa marehemu alikuwa mtumishi mwadilifu, mchapakazi na aliyetoa mchango mkubwa katika kuimarisha usimamizi wa masuala ya fedha na uwajibikaji ndani ya taasisi hiyo.
Mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa kwa ushirikiano kati ya familia ya marehemu na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, huku taarifa zaidi kuhusu ratiba ya mazishi ikitarajiwa kutolewa baadaye.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watumishi wote walioguswa na msiba huo, ikiwaomba waendelee kumuombea marehemu apumzike kwa amani.



