Home KITAIFA Nkasi yajengewa uwezo masuala ya menejimenti ya maafa

Nkasi yajengewa uwezo masuala ya menejimenti ya maafa

Na Mwandushi Wetu, Nkasi

IDARA ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu imewajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Wataalamu ya Usimamizi wa Maafa ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa ili kuhakikisha jamii inakuwa stahimilivu wakati wa majanga.

Elimu hiyo imetolewa leo Januari,19 2026 na timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa kikao cha kupitia Rasimu za Nyaraka za Usimamizi wa Maafa za Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa Kamati za Usimamizi wa Maafa wilayani humu ikiongozwa na na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo.

Kikao hicho kimeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na timu ya wataalamu kutoka ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kikilenga kuwapitisha katika nyaraka zilizoandaliwa kwa ajili ya matumizi ya Halmashauri ambazo ni Tathmini ya Vihatarishi vya Majanga, Uwezekano wa Kuathirika na Uwezo wa Kukabiliana na Majanga, Mpango wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa pamoja na Mkakati wa kupunguza vihatarishi vya maafa.

Akitoa neno la shukran mara baada ya kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Eliud Njogellah amepongeza kazi iliyofanyika na timu ya kuandaa nyaraka hizo huku akieleza kuwa zimekuja kwa wakati sahihi ambapo Halmashauri imekuwa ikikumbwa na majanga na maafa mbalimbali hivyo zitatumika kwa uzito wake na tija iliyokusudiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here