Home KIMATAIFA Gachagua adai kulikuwa na jaribio la kumuuwa kanisani

Gachagua adai kulikuwa na jaribio la kumuuwa kanisani

Na Mwandishi Wetu

MWANACHAMA maarufu wa upinzani nchini Kenya Rigathi Gachagua amedai kulikuwa na jaribio la kumuua wakati wa ibada ya siku ya Jumapili kanisani.

Gachagua ambaye aliondolewa kwenye wadhifa wake kama Naibu wa rais mwaka 2024, alidai kundi la maafisa wa polisi wasio na nidhamu walishambulia kanisa huko Othaya katika kaunti ya kati ya Nyeri, kwa kutumia risasi na gesi ya machozi.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen amelaani vurugu hizo, akiziita hazikubaliki.

Polisi imetangaza kufunguliwa kwa uchunguzi na kuthibitisha kwamba hakuna majeraha yaliyoripotiwa.

Kulingana na ripoti za polisi, bomu la machozi linadaiwa kutupwa ndani ya Kanisa la Anglikana la St. Peter saa 11:00 asubuhi kwa saa za huko, na kukatiza ibada huku Magari kadhaa yakiripotiwa kuharibiwa katika uwanja wa kanisa

Polisi Kenya wametoa wito kwa watu wenye ushahidi usio na shaka ili kusaidia kubaini chanzo cha tukio hilo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here