Home KITAIFA Waziri Mkuu azindua miradi ya shilingi bilioni114 ya utalii

Waziri Mkuu azindua miradi ya shilingi bilioni114 ya utalii

Na Mwandishi Wetu,Pwani

WAZIRI Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amezindua na kukabidhi miundombinu 21 ya utalii yenye thamani ya Shillingi billioni 114.62.

Amesema ujenzi wa Miradi hiyo ambayo imejengwa kupitia mradi wa kimkakati wa kukuza na kuendeleza utalii ukanda wa Kusini ni sehemu ya maono ya Dkt. Samia Suluhu Hassan yanayolenga katika kukuza sekta ya utalii nchini.

Amesema hayo leo Jumatano Februari 11, 2026 wakati alipozindua uwanja wa ndege Mtemere uliopo katika kijiji cha Mloka, mkoani Pwani kwenye hifadhi ya Taifa ya Nyerere. Uwanja huo ni sehemu ya miradi 21 iliyozinduliwa.

Dkt. Mwigulu ameitaja miradi hiyo kuwa ni Malango ya kuingilia Hifadhini, vituo vya taarifa kwa wageni, kambi za wageni, Eneo la Kupumzikia wageni, Nyumba za wageni, Hosteli za Wanafunzi, kituo cha kufuatilia ikolojia, na vituo vya askari.meziagiza mamlaka zote zihakikishe zinaitunza na kuilinda Miundombinu hiyo ambayo imegramu fedha nyingi.

“Hakikisheni miradi hii inatunzwa na kukarabatiwa mara kwa mara ili kuwezesha nchi kufikia malengo ikiwemo kuongeza pato la utalii na kutoa ajira, Wananchi hakikisheni pia mnailinda miundombinu hii,”amesema.

Ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana na Mashirika ya Ndege ikiwemo ATCL ili kuona namna bora ya kutumia fursa ya ujenzi wa uwanja na kuandaa ratiba za ndege Kutoka Dar/Zanzibar – Nyerere – Mikumi-Ruaha-Songwe.

Pia, Dk. Mwigulu amesema kuwa Serikali imeendelea kuwekeza katika miundombinu mbalimbali ikiwemo ununuzi wa magari 61 kwa ajili ya shughuli za utalii na doria.

“Vilevile, Serikali imenunua jumla ya mitambo mikubwa 18, malori 46, matrekta 7 na vifaa vingine mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza sekta hii ya uhifadhi na utalii.

Tutaendelea pia kuweka mazingira wezeshi na rafiki katika kuendeleza sekta ya utalii na uhifadhi kwa kuweka sera ambazo zitawezesha sekta binafsi kuwekeza zaidi katika uhifadhi na utalii kwa maslahi mapana ya Taifa,”amesema

Awali, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Ashatu Kijaji amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt. Samia idadi ya watalii imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 149 ikiwa ni ongezeko la watalii 2,294,495 mwaka 2025 kutoka watalii 922, 692. “ongezeko hili limetokana na uwekezaji mkubwa na wakimkakati katika sekta ya uhifadhi na utalii”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here