Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imesema katika siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan wametoa msamaha wa matibabu wenye gharama ya Sh milioni 100 kwa wagonjwa 1,306 ikiwa ni pamoja na watu waliopoteza maisha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari, 18 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Balozi Dk. Mpoki Ulisubisya amesema katika siku hizo wagonjwa waliopa huduma ni 54,594 wamepata katika yao 1,644 wamepata huduma za kupasualiwa na wagonjwa 19,281 wamepata huduma za vipimo kama X -ray ,Ultrasound na mengine ambapo imepunguza tufaa nje ya nchi.
“Mambo tuliyofanya siku 100 za Dk Samia kumekuwa na uhitaji wa kupanua wigo wa aina ya uchunguzi na tumeongeza huduma ya kufanya uchunguzi kwa njia ya matundu mgonjwa mgonjwa anaigizwa kwenye mashine maalum anapigwa picha Daktari kuona anatatizo sehemu gani huko nyuma tulikuwa tunapasua.
Amesema kitu kipya kingine walichofanya ni kuweka simenti tiba katika pingili za mifupa ya mgongo ambavyo vikiwekwa vinarudi jinsi zilivyokuwa.
“Kwa kipindi kirefu hawa wagonjwa walikuwa hawana afua maalum siku 100 tulipata madaktari wanaohudumia wenye maumivu sugu sasa wanapata matibabu na watu 22 wameshanufaika na tiba hii ,”amesisitiza Balozi Dk. Mpoki.
Amesema hivi sasa wanautaratibu wa kurekebisha viungo vilivyopooza mfano mikono au miguu na waangalia mishipa ya fahamu inarekebishwa ambapo mtu ataweza kutumia viungo vyake.
“Kwa muda mrefu tumekuwa tukiongelea hiduma za utengamao hii ni sehemu ya watu waliopata kiharusi au kupata ajali zilizohar8bu baadhiru ya sehemu ya mwili.
Amesema kutokana na changamoto la ongezeko la wagonjwa na uhitaji wa wodi binafsi hivi sasa wameongeza wodi 25 vya watu binafsi. Aidha ameeleza kuwa kutokana na ongezeko la foleni kubwa ya wagonjwa
Wamekuja na njia ya kuweka miadi kwa njia ya mtandao ambapo mgonjwa atachagua daktari ambaye anataka amuone hata wa nje ya nchi wanaweza kufanya hivyo.
“Tumeanza utaratibu wa kutoa tiba kupitia wino maalumu ambayo mgonjwa anawekewe na daktari kupitia miwani maalum anaweza kuona ugonjwa katikaa mfumo wa fahamu ulivyoenea.
Ameongeza: “MOI inaweza ikatibu asilimia 98 za magonjwa ya mifupa yanayoweza kumpata mtu asilimia 97 ni magonjwa na mishipa ya fahamu tumejaribu kupunguza na kufikia asilimia 99 hadi 100.
Dk Mpoki amesema wanaendelea kutekeleza wajibu wa jamii kupata mafunzo kuhusu suala la bima na wanawaelimisha wajiunge,wanamikakati ya kuboresha huduma wanawafundisha watumishi utoajia huduma na kuwaambia wagonjwa haki zao.
Pia amesema wanapeleka huduma karibu na jamii ikiwmo hospitqli ya Chato wana madaktari wao wako muda wote.
“Tunatoa huduma katika hospitali ya Mwalimu Nyerere kule Musoma
Tutaenda na sehemu nyingine kama mikoa ya Arusha itaenda pale Arusha Lutheran Medical Centre tutashirikiana na JKCI tutakwenda kigoma,katavi na mikoa mingine ya nchi hii ,”amesisitiza Dk Mpoki.



