Na Mwandishi wetu
MABONDIA maarufu duniani Manny Pacquiao na Floyd Mayweather wamekubaliana kurudi ulingoni kuzichapa tena katika pambano la kitaalamu linalotarajiwa kufanyika mwezi Septemba, mwaka huu.

Pacquiao mwenye umri wa miaka (47), na Mayweather, (48), watapigana huko Las Vegas Jumamosi, ya Septemba 19, huku pambano hilo likionyeshwa moja kwa moja kwenye Netflix.
Itakuwa pambano la kwanza la kitaalamu kwa Mmarekani huyo tangu amshinde Conor McGregor raundi ya 10 ya pigano kwa ‘knockout’ tangu mwaka 2017.
Pacquiao wa Ufilipino alistaafu kutoka kwenye mchezo huo ili kujikita zaidi kwenye taaluma yake ya kisiasa mwaka 2021 lakini alirudi ulingoni Julai iliyopita kupambana na bingwa wa WBC wa uzito wa welterweight Mario Barrios, ambaye alihifadhi taji lake baada ya kutoka sare.
Mayweather na Pacquiao walikutana kwa mara ya kwanza mwaka wa 2015, katika kile kilichoitwa Pambano la Karne na linasalia kuwa la kihistoria katika ndondi.
Mayweather aliibuka na ushindi, akimshinda Pacquiao kupitia uamuzi mpana wa pamoja huko Las Vegas.
Pacquiao, mshindi wa mataji 12 ya dunia katika madaraja manane ya uzito, alisema: “Mimi na Floyd tuliipa dunia pambano kubwa zaidi katika historia ya ndondi.”
“Mashabiki wamesubiri vya kutosha. Wanastahili mechi hii ya marudiano.”
“Nataka Floyd aishi na majuto ya pambano alilopoteza katika rekodi yake ya kitaaluma na akumbuke kila wakati ni nani aliyempa kipigo hicho.”
Mayweather, ambaye anatimiza miaka 49 siku ya Jumanne, alisema: “Tayari nimepigana na kumshinda Manny mara moja. Wakati huu matokeo yatakuwa sawa.”
Mayweather ameshinda mapambano yake yote ya kitaaluma kwa 50-0, huku 27 akishinda kwa ‘knockout’.
Chanzo BBC



