Home KIMATAIFA Dk. Biteko ateta na Spika wa Bunge Morocco

Dk. Biteko ateta na Spika wa Bunge Morocco

📌 Tanzania, Morocco wakubaliana kuimarisha ushirikiano

Morocco

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ametembelea Bunge la Morocco ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini humo.

Akiwa Bungeni hapo, Dk. Biteko amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la nchi hiyo Mh Rachid Talbi El Alami na Naibu Spika Lahcen Haddad katika ofisi za Bunge hilo zilizoko jijini Rabat nchini Morocco.

Pamoja na mambo mengine, wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika Sekta ya Nishati, Kilimo, Viwanda na Biashara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here