Dar es Salaam
WAZIRI Mkuu,Kassim Majaliwa leo Juni 01, 2025 jijini Dar es Salaam amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika tuzo za wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa zinazoandaliwa na Baraza la Michezo Taifa.

Lengo la tuzo hizo ni kuwaenzi na kuwatambua watanzania wanaiowakilisha nchi katika michezo mbalimbali duniani na kuiletea sifa Tanzania kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza Katika hafla hiyo, Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita itaendelea kuwekeza katika sekta ya michezo kwa kuwa inatambua michezo ni afya, ajira, mshikamano, maendeleo lakini pia michezo ni burudani.

Katika hafla hiyo Majaliwa alipokea kwa niaba ya Rais Dk. Samia tuzo ya kutambua mchango wake katika kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini.
Aidha, pia Majaliwa alikabidhiwa tuzo ya kutambua mchango wake katika kusimamia michezo nchini.