Home KITAIFA Waziri Mkuu aagana na Balozi wa Angola aliyemaliza muda wake nchini

Waziri Mkuu aagana na Balozi wa Angola aliyemaliza muda wake nchini

▪️Ampongeza kwa kutumikia nchi yake kwa mafanikio makubwa ya kidiplomasia nchini.
▪️Balozi de Oliveira asema Angola itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Tanzania.
 
Na Mwandishi wetu, Dodoma

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 28, 2025 amemuaga rasmi Balozi wa Angola nchini Tanzania, Sandro Agostinho de Oliveira, ambaye anamaliza muda wake wa uwakilishi baada ya kutumikia nchi yake kwa mafanikio makubwa ya kidiplomasia nchini.

Majaliwa ambaye ameagana na Balozi huyo jijini Dodoma kwa niaba ya Rais Dk. Samia Suluhu, amempongeza Balozi de Oliveira kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, kisiasa na kijamii kati ya Tanzania na Angola.

Amemweleza balozi huyo kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuthamini na kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia na kidugu kati ya Tanzania na Angola katika nyanja zote muhimu za maendeleo.

Balozi de Oliveira ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mzuri alioupata wakati wote wa uwakilishi wake na amesema kuwa Angola itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Tanzania katika kuendeleza ustawi wa nchi hizo mbili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here