Home BIASHARA UDSM yaja na bajaji inayotumia maji na mafuta

UDSM yaja na bajaji inayotumia maji na mafuta

*Uwepo wa mfumo wa maji katika bajaji unatajwa kuwa moja ya njia inayoweza kupunguza gharama za uendeshaji kwani injini inapopoa hutumia mafuta kidogo


Dar es Salaam.

WAKATI biashara ya usafirishaji inavyozidi kukua nchini, watu wameendelea kubuni namna rahisi ambazo zitawawezesha watu kufanya shughuli zao kwa urahisi.

Hiyo ni kwa kuwatafutia suluhisho la linaloweza kuwapunguzia gharama za uendeshaji.

Hilo limeoneka kwa Andrew Mbanga kutoka ndaki ya Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET) Ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye amekuja na bajaji inayotumia maji na mafuta.

Amesema kwa mara ya kwanza alitengeneza bajaji ya aina hiyo mwenyewe lakini alipoambiwa kupeleka chuo Kikuu cha Dar es Salaam ifanyiwe marekebisho ilibainika kuwa imekaa muda mredu baada ya kufanyisa vipimo.

Ameyasema hayo alipozungumza na Lajiji Digital Julsi Mosi, 2025 katika maonyesho ya 49 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yaliyoanza Juni 28 na yanatarajiwa kukamilika Julai 13 mwaka huu.

“Hivyo ilibidi tuanze upya kwa kwa kushirikiana na wahandisi wa chuoni hapo, kitu kimoja baada ya kingine hadi tulipoikamilisha inavyoonekana leo,” amesema Mbanga.

Akielezea inavyofanya kazi, Mmbaga amesema bajaji hiyo ina mfumo wa kuingiza maji kwa ajili ya kupooza ‘cylinder’ zisipate moto ambapo maji huwekwa katika tanki maalumu.

“Maji hayo huja kwenye injini yakiwa ya moto huingia katika rejeta na ile feni iliyo katika rejeta inafanya maji yapoe na kuanza mzunguko mpya. Hilo linafanya injini inapoa muda mwingi hali inayofanya mafuta kidogo kutumima ukilinganisha na mfumo huo ungekosena,” amesema.

Amesema maji yanayotumika ni safi yoyote isipokuwa yasiyokuwa ya chumvi na hufanya kazi kwa wiki moja na mtu anatakiwa kubadilisha ikiwa mtu anafanya kazi kila siku.

“Ukiacha yachafuke sana yataziba matundu ya rejeta kwa sababu maji yanapozidi kuwa ya moto sana yanatengeneza povu, sasa povu likiendelea kukaa ndani ya rejeta na ikiwa ni maji ya chumvi ndiyo kabisa yanaziba matundu,” amesema.

Amesema bajaji za abiria za kawaida hazina mfumo wa maji isipokuwa zile za mizigo huku akisema lengo ni kufungua kiwanda cha kutengeneza bajaji.

“Tutakuwa tunatengeneza bajaji aina tatu, ya kutumia gesi, bajaji za umeme jua na bajaji za kutumia mafuta ya kawaida,” amesema Mbanga.

Amesema wanatazamia kufanya biashara na watu wa ndani na nchi za jirani na sasa anaikiri tayari kupata oda za watu wanaotaka kutengenezewa bajaji hizo.

“Tukimaliza sabasaba tutakwenda Costecj ili bajaji iweze kuthamini na baadaye itaingia katika majaribio rasmi barabarani, baada ya uthamini tutaweza kupanga bei ambayo mteja anaweza kulipia,” amesema.

Mmoja wa watembeleaji ambaye pia alikuwa akipate maelezo juu ya bajaji hiyo, John Julius amesema uwepo wa bunifu kama hizo unasaidia kurahisisha shughuli za kiuchumi.

“Kama ni mafuta kidogo mtu anakuwa na uhakika wa kipato, hii itaimarisha uchumi wa familia nyingi ukizingatia eneo hili limeajiri vijana wengi,” amesema.

Maneno yake yaliungwa mkono na Sabato Masanja ambaye alitaka bunifu zinazoweka urahisi katika baadhi ya maeneo kuangalisa kwa jicho la kipekee ikiwemo mikopo au ufadhili.

“Kungekuwa na utaratibu wa kuhakikisha watu kama hawa ndiyo wanapewa fedha kwanza ili waendeleze bunfu zao kusaidia wengune wanaowazunguka,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here