Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini imetoa rai kwa wananchi kujitokeza kwenye maonesho ya 49 ya biashara sabasaba ili kupata elimu ya sheria zinazosimamiwa na ofisi hiyo hasa katika kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi mkuu 2025.

Akizungumza na Lajiji Digital julai 3,2025 Afisa Sheria wa OfisiDinna Mcharo amesema ofisi hiyo inasimamia sheria mbalimbali za vyama vya siasa ikiwemo sheria ya vyama vya siasa sura ya 258 lakini pia sheria ya gharama za uchaguzi sura ya 278.
“Mimi nitoe rai kwa wananchi wanaokuja kutembelea maonesho haya kuhakikisha wanapita hapa ili waje wapate elimu wajue sheria ziazowasimamia wanasiasa kipindi wanapotekeleza majukumu yao ya kisiasa hasa tunapoelekea uchaguzi mkuu,”amesema.
Amesema wameshiriki katika maonesho hayo ili kuendelea kutoa elimu kwa umma ili wapate kujua sheria zinazosimamiwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kuu.
Ameongeza kuwa ofisi ya msajili wa vyama inamajukumu mengi ikiwemo kusajili na kufuatilia utendaji wa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria lakini piakuratibu shughuli za baraza la vyama vya siasa.
Pia wanajukumu la kufuatilia mapato na matumizi ya vyama vya siasa lakini kugawa na kufuatilia matumizi ya fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa vyenye sifa.