Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sagini, ameelezea siri iliyochangia Wizara hiyo kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Wizara kwenye maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF) Sabasaba kuwa ni elimu bora ya msaada wa kisheria inayotolewa na Maofisa na wanasheria ikilenga kutatua changamoto na migogoro za wananchi hao.

Akizungumza Julai, 8 2025 jijnini Dar es Salaam Naibu Waziri Sagini kwenye maonesho hayo amewataka wananchi kutembelea banda la Katiba na Sheria ili kupata elimu inayohusu masala ya Sheria.
Ameishukuru Serikali inayoingozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya maboresho yaliyofanywa katika viwanja hivyo.
“Licha ya migogoro ya Ardhi,pia kuna migogoro ya ndoa ambapo Elimu inatakiwa kutolewa kwa kushirikiana na maafisa walipo kwenye Mamlaka ngazi za Mitaa na wataalamu wa msaada wa kisheria waliopo ambao ni wadau wa huduma za msaada wa kisheria kwa kuelimisha wananchi kuhusu ndoa,” amesema.
Akizungumzia Banda la Katiba na Sheria, Sagini amesema wanastahiki kuwa washindi wa kwanza ambapo wananchi wameridhishwa na utolewaji wa huduma.

“Niwapongeze wataalamu Wetu, mawakili wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria niwapongeze Waziri na Katubu Mkuu kukubali kuleta Idara zoteza Katiba Sheria hapa ambao pia hutoa Elimu ya masala mbalimbali ya yanayoratibiwa na hizo Idara,”amesema.
Akizungumzia kampeni ya Msaada wa kisheria, Sagini amesema huduma hiyo imeleta matokeo chanya ambapo serikali imeridhishwa na utolewaji wa huduma hiyo.
“Wizara ya Katiba na Sheria inalifanya jambo hili kuwa endelevu kwa kupeleka maafisa ngazi ya Halmashauri ambapo wanawasaidia wananchi kwa kushirikiana na taasisi zingine za kisheria,”amesema.

Ameongeza kuwa wameweka kipaumbele kutoa elimu kwa wananchi kuhusu sekta kama ardhi.
Akiwa kwenye maonesho hayo ametembelea Banda la Mahakama, Wakala wa Vizazi na Vifo(RITA) ambapo amebaini ushiriki wa watu wengi waliojitokeza kuomba vyeti vya kuzaliwa.

Amesema wananchi wanapaswa kufahamu kuwa huduma ya utoaju wa vyeti upo hadi ngazi za Wilaya hivyo hakuna sababu ya kusubiri wakati wa maonesho ya Sabasaba ambapo wengine hukutwa vyeti vyao vimeshapelekwa kwenye Wilaya wanapotoka.