Home KITAIFA TPTC kimeendelea kuaminika na medani za Umoja wa Mataifa

TPTC kimeendelea kuaminika na medani za Umoja wa Mataifa

Na Esther Mnyika, Dar es Salaam

CHUO cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania (TPTC) kimeendelea kuaminika na medani za Umoja wa Mataifa (UN) katika kujitoa kwenye misheni mbalimbali za kijeshi za ulinzi wa amani.

Hayo amebainisha leo Julai,17 2025 Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Huduma za Tiba Jeshini, Meja Jenerali Amri Mwami wakatiwa kufunga mafunzo ya Maafisa Wanadhimu wa Umoja wa Mataifa (UNSO TOT) ambapo yameshirikisha maafisa wakufunzi kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Amesema Mafunzo hayo yalikuwa ni ya Wiki mbili ya walimu walioandaliwa kwaajili ya kwenda kufundisha katika nchi zao.pia ni maboresho na miongozo mbalimbali inayotolewa na Umoja wa Mataifa kutokana na uzoefu uliopatikana katika kushiriki mafunzo ya ulinzi wa amani sehemu mbalimbali katika Afrika.

“Mafunzo ya wiki mbili yanalenga kudumisha amani na chuo hichiTanzania kimezidi kuaminika kufundisha kozi hizi za kimataifa jambo ambalo ni heshima kwa taifa,” amesema Meja Jenerali Mwami.

Amesema Waliohitimu leo watakwenda kutumia maboresho ilitolewa na UN ili kuboresha utoaji wa huduma za ulinzi na amani ziwe Salaam na kiweledi zaidi.

Ameongeza kuwa jukumu kuu la Umoja wa Mataifa ni kuhakikisha amani inadumu na duniani na kuwa bora na mahali bora pakuishi.

Naye Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wwa Amani (TPTC), Bregedia Jenerali George Itang’are MWIT amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo maafisa wakufunzi ambao watakao fundisha maafisa wanadhimu wa umoja huo ili wawezekutekeleza majukumu yao
kwa ufanisi na weledi.

Amesema mafunzo hayo yamewaleta pamoja jumla ya maofisa 22 kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Ghana, Nigeria, Tanzania, Vietnam, Botswana, na Zambia na wakufunzi saba kutoka Tanzania,Brazil, Bangladesh, Nigeria na Marekani.

Amefafanua kuwa mafunzo hayo yanaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Canada, ambayo imetoa msaada wa kifedha kufanikisha mafunzo hayo, ikiwemo kugharamia usafiri, malazi na chakula kwa washiriki.

Naye Mratibu wa Mafunzo wa Umoja wa Mataifa kutoka Nigeria, Kanali Ibrahim Abdul amesema wamewafundisha na kuwajengea uwezo maafisa na wakufunzi ili wanapopelekwa kwenye utekelezaji wa misheni kuwa na uwelewa.

Kwa upande wake Balozi wa Canada nchini Tanzania,Emily Burns amesema licha ya kufadhili mafunzo hayo bado wanaamini ushirikiano mzuri na Tanzania hasa katika kujitoa kulinda amani huku maafisa wakufunzi wanaimarika kiuwelewa na matumaini ya Umoja wa Mataifa na dunia kuwa na amani na ulinzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here