Home KITAIFA MEO na DMTA wasaini makubaliano ya ushirikiano kusaidia vijana ajira kwenye sekta...

MEO na DMTA wasaini makubaliano ya ushirikiano kusaidia vijana ajira kwenye sekta ya meli

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

TAASISI Maritime empowment Organization imesaini makubaliano ya miaka mitatu ya kukuza ushirikiano na DMTA Crewing Angecy ikiwa lengo ni kuwawezesha vijana kupata ajira sekta ya meli ndani na nje ya nchi.

Akizungumza leo Julai, 18 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini Mkurugenzi Mkuu wa Crewing Agency, Capt. Ken Chimwejo amesema makubaliano hayo yana malengo mawili ni pamoja na kuwajengea uwezo vijana waliomaliza mafunzo ya bahari kuputia MEO.

Amesema lengo la pili kupanua wigo wa kusaidia vijana wa kitanzania kupata ajira kwenye mashirika na Kampuni za meli ndani na nje ya nchi kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuchangia Pato la Taifa.

“Kazi za meli zinahitaji mafunzo kama sekta zingine hivyo kijana lazima apate mafunzo hivyo mwitiko wa vijana kufanya kazi kwenye meli ni mkubwa,”amesema.

Ameongeza kuwa hadi sasa takwimu zinaonesha vijana 78 wamefikiwa na na ajira hizo tangu kuanzishwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti, Eliyusta Filikunjombe ushirikiano huo ni hatua muhimu katika kuboresha sekta ya baharini na kutengeneza fursa zaidi za ajira kwa vijana wa Tanzania.

Amesema kutokana na changamoto ya ajira makubaliano hayo yatapunguza changamoto hiyo kwa sababu vijana watakuwa wamepata fursa ya ajira kwenye sekta ya baharini hususani katika soko la Kimataifa.

“Tumeungana kuongeza juhudi katika kusaidia kutokomeza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na kuwekeza katika sekta ya uchumi wa buluu, “amesema Filikunjombe.

Ameto wito kwa vijana nchini wataendelea kuwawezesha kwa mafunzo, mazingira rafiki ya viwango vya kimataifa ili wapate nafasi za ajira duniani.

Kwa upande wake Capt. Abdulaleem Bapumia amesema amefanya kazi za meli za nje ubaharia zaidi ya miaka 20 umuhimu wa kazi hiyo wanahitaji kuwa wavumili kwasababu fursa zipo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here