Home KITAIFA TANESCO yazindua mfumo wa kupokea taarifa za siri

TANESCO yazindua mfumo wa kupokea taarifa za siri

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limezinduzi rasmi Mfumo wa Kupokea taarifa za siri, maarufu kama “Whistleblower portal”, unaolenga kulinda watoa taarifa dhidi ya vitisho na kulinda maadili.

Akizungumza leo Agosti,4 2025 jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugezi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja TANESCO, Irene Gowele amesema mfumo huo umeanzishwa kurahisisha upokeaji wa taarifa kutoka kwa wananchi.

“Kwa kipindi kirefu TANESCO imekuwa ikipata changamoto mbalimbali zinazowakwamisha wakati mwingine dhidi ya utoaji wa huduma endelevu ya umeme kama vile wizi na uharibifu miundombinu ya umeme, vitendo vya rushwa kutoka kwa baadhi va watumishi wasio waamijifu na upotevu wa mapato unaotokana na uharibifu wa miundombinu ya umeme unaoweza kuzuilika mapema, ” amesema.

Amesema mfumo huo kurahisisha upokeaji wa taarifa kutoka kwa wafanyakazi wa TANESCO na wadau wengine kuhusu vitendo vya wizi wa mali za shirika, rushwa hujuma za uharibifu wa miundombinu ya umeme na vitendo vya unyanyasaji vivyofaa katika mazingira ya kazi.

Irene amesema ujio wa mfumo huu mpya ni hatua muhimu ya kimageuzi katika utendaji kazi wa shirika hilo na unalenga kuimarisha uwajibikaji, kudhibiti uhalifu, kulinda watoa taarifa dhidi ya vitisho na kuuongeza uaminifu wa umma kwa TANESCO.

“Mtoa taarifa ataelekezwa hatua stahiki na taarita itachukuliwa kwa usiri mkubwa. Kupita mfumo huu, Shirika linauhakikishia umma kuwa taarita zote zitakazopokelewa zitatunzwa kwa usiri mkubwa na kushughulikiwa,” amesema.

Ameongeza kuwa mfumo utakuwa na faida kubwa kwani utazuia vitendo hivyo kwa sababu umetengenezwa kwa siri, Watanzania watumie kwani ni mwepesi na ni sehemu ya uboreshaji wa huduma na mwendelezo wa kampeni ya lipa deni iliyotangazwa kwa wenye madeni marefu.

Aliwahimiza wananchi wote kushiriki kikamilifu kwa kuutumia mfumo huo kusaidia kulinda rasilimali na maslahi ya Shirika na Taifa kwa ujumla na kuimarisha huduma kwa wateja na kuongeza ufanisi wa ndani wa Shirika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here