Home KITAIFA Tanzanian nchi ya kwanza duniani kuleta teknolojia ya DNA kwenye sekta...

Tanzanian nchi ya kwanza duniani kuleta teknolojia ya DNA kwenye sekta ya kilimo

Na Esther Mnyika , Dodoma

TANZANIA imekuwa nchi ya kwanza duniani kuingiza teknolojia mpya ya Vipimo vya Vinasaba (DNA) katika sekta ya kilimo kwaajili ya kubaini visumbufu mbalimbali vinavyo athiri uzalishaji wa mazao hapa nchini yakiwamo magonjwa na wadudu waharibifu wa mazao.

Hayo ameyasema Agosti 6,2025 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Profesa Joseph Ndunguru, wakati akizindua Teknolojia hiyo maonesho ya Wafugaji na wakulima ‘nane nane’ ambayo yanafanyika kitaifa jijini Dodoma.

Baada ya kuzindua teknolojia hiyo amesema kuwa hiyo ni teknolojia ya kisasa ambayo inatoa majibu ndani ya dakika 20 huko huko shambani kwa mkulima bila kuhitaji kwenda maabara.

“Leo hii katika viwanja vya maonesho haya ya nane nane tumezindua teknolojia mpya ya vipimo vya vinasaba (DNA), ambayo inaenda kusaidia kutoa majibu ya visumbufu vinavyo athiri uzalishaji wa mazao hapa nchini yakiwamo magonjwa na wadudu waharibifu wa mazao,” ameeleza.

Profesa Ndunguru amesema teknolojia hiyo inaenda kuwahakikishia kukidhi viwango, mahitaji ya masoko ya kimataifa kwa sababu mazao ambayo watakuwa wakiyapeleka kwenda nje ya nchi yatakuwa ni mazao ambayo yamethibitishwa bila wasi wasi hayana visumbufu vyovyote.

Ameongeza kuwa teknolojia hiyo inaenda kuwapatia uhakika wa kufanya biashara na mataifa ya nje ambapo nchi itapata Pato na wananchi watakipatia kipato kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi.

“Mbali na matumizi kwenye sekta teknolojia hik ina matumizi mengine katika sekta mbalimbali ikiwamo mifugo,afya ya binadamu, kuhifadhi anwani hivyo ni teknolojia nzuri wakulima pamoja na Watanzania wategemee teknolojia hii inaenda kuwaletea tija,” amesema.

Aidha amewakaribisha wadau wa mbegu,miche na Watanzania katika Mamlaka hiyo kwenda kupata huduma ambapo teknolojia hiyo itawaonesha ubora wa mbegu hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here