Home SIASA Wasira: CCM chama. Kikubwa hakiwezi kugombana na Mpina

Wasira: CCM chama. Kikubwa hakiwezi kugombana na Mpina

Na Mwandishi wetu, Simiyu

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema CCM haina ugomvi na aliyekuwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, kwa kuwa Chama kikubwa hakiwezi kugombana na mtu binafsi.

Wasira ameeleza hayo Septemba, 7 2025 wilayani Kisesa Mkoa wa Simiyu, alipokutana na viongozi na wanachama wa CCM katika kikao cha ndani kuvunja makundi na kuwaweka pamoja wana CCM ili kuwa na nguvu ya pamoja kusaka ushindi wa mgombea urais Dk. Samia Suluhu Hassan, wagombea ubunge na udiwani wa mkoa huo.

“CCM Chama kikubwa sana katika Afrika, wengine wanakuja kutuuliza nyinyi mnaendeleaje, halafu wasikie eti Chama kinagombana na Mpina, hapana, sisi hatuna ugomvi na Mpina.

Ndugu zake Mpina mleeni Mpina kiakili wakati atakapokuwa amekosa urais ili aendelee kuwa mtu mzuri na mwanakijiji wa Mwandoya mzuri. Kazi ya kumlea itakuwa ya familia na majirani zake kwa sababu urais hawezi kupata tunajua.

Pia hatumwambii ukikosa urudi ni hiyari yake vilevile, ila akirudi tutampokea, lakini hatumwambii lazima urudi maana si lazima awe rais anaweza kuwa mwanachama wa kawaida wa chama chake kipya, lakini ana kazi kweli maana hapa Kisesa mwanachama wa hicho chama chake kipya ni yeye mwenyewe,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here