Home KIMATAIFA Mvutano Marekani na Venezuela wazidi kushika kasi

Mvutano Marekani na Venezuela wazidi kushika kasi

Washingiton, Marekani

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema jeshi la nchi yake limeharibu meli inayodaiwa kuwa ya mihadarati kutoka Venezuela, iliyokuwa ikielekea Marekani kupitia bahari ya kimataifa.

Akizungumza Jumatatu, Trump alisema wanaume watatu waliuawa katika shambulizi dhidi ya kile alichokitaja kuwa “makundi ya ulanguzi wa dawa za kulevya”. Hata hivyo, hakutoa ushahidi kuthibitisha kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba dawa za kulevya.

Muda mfupi kabla ya kauli hiyo, Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, alionya kuwa Caracas itajilinda dhidi ya kile alichokiita “uchokozi wa Marekani”. Aidha, alimshutumu mwanadiplomasia wa Marekani, Marco Rubio, akimtaja kama “mbabe wa vifo na vita”.

Mvutano kati ya mataifa hayo mawili umeongezeka baada ya Marekani kupeleka meli za kivita katika Bahari ya Caribbean kusini kwa kile maafisa wake walisema ni operesheni za kupambana na mihadarati. Hatua hiyo ilifuatwa na shambulizi lililoripotiwa kusababisha vifo vya watu 11.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here