Home KITAIFA Makamu wa Rais kushiriki mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa...

Makamu wa Rais kushiriki mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa – Marekani

Na Mwandishi wetu

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango, leo Septemba, 20 2025 ameondoka nchini kuelekea New York, nchini Marekani kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA 80).

Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinachoshirikisha Wakuu wa Nchi na Viongozi mbalimbali ni Mkutano muhimu ambao, pamoja na mambo mengine, hujadili masuala ya kiuchumi, kisiasa na haki za binadamu.

Kikao hicho kinafanyika chini ya Kaulimbiu isemayo “Tuko Vizuri tukiwa pamoja: Miaka 80 na Zaidi kwa Amani, Maendeleo, na Haki za Binadamu” (Better Together: 80 Years and Beyond for Peace, Development, and Human Right). Kaulimbiu hiyo ni wito wa pamoja wa kuimarisha Umoja wa Mataifa ili uweze kukabiliana vyema na changamoto za sasa na zile zinazokuja, huku ukilinda mafanikio yaliyopatikana.

Aidha, Makamu wa Rais anatarajiwa kuhutubia Kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pamoja na kushiriki kwenye vikao mbalimbali ikiwemo Mjadala Mkuu (General Debate), Mikutano ya pembezoni na Mikutano ya uwili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here