Home SIASA DK.Samia: Tutajenga barabara ya tabaka gumu Ngorongoro kwenda Serengeti

DK.Samia: Tutajenga barabara ya tabaka gumu Ngorongoro kwenda Serengeti

Na Mwandishi wetu,Arusha

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema ikiwa Watanzania watampa ridhaa ya kuunda serikali yake itaenda kuziunganisha Wilaya za Ngorongoro na Monduli kwa kiwango cha Lami pamoja na ujenzi wa barabara nyingi ndani ya Wilaya hizo katika kurahisisha shughuli za Kijamii na Kiuchumi katika Wilaya hizo za Mkoa wa Arusha.

Dkt. Samia amebainisha hayo leo Ijumaa Oktoba 03, 2025 Mbele ya Mamia ya wananchi wa Karatu Mjini kwenye Viwanja vya Mnadani ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Kampeni zake kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akisema Miongoni mwa barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami ni barabara ya Engaruka- Ngaresero (Km 24) ambapo usanifu umekamilika na sasa wapo kwenye hatua za kuweza kutangaza zabuni.

“Ujenzi wa barabara ya Selela- Engaruka (Km 17) na kubainisha kuwa kinachofanyika sasa ni kutangaza zabuni na kumpata mkandarasi wa kujenga barabara hiyo muhimu itakayounganishwa na Kiwanda cha Magadi soda, ikitumika pia kwaajili ya Utalii katika Ziwa Natron Wilayani Monduli,”amesema.

Kwa upande wa Karatu, Dkt. Samia ameahidi ujenzi wa barabara ya kutokea Geti la Ngorongoro kuelekea Serengeti (Km88) zikijengwa kwa tabaka gumu, barabara ambayo itajengwa kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza itagharimu shilingi Bilioni 70 na ujenzi wake ukitarajiwa kuanza kwenye mwaka huu wa fedha.

Pia ameahidi pia kufanyia kazi ombi la ujenzi wa Kilomita kumi za barabara kuelekea kwenye maeneo zilipo hoteli za Watalii Wilayani Karatu, akitangaza pia kufunga taa za barabarani kuanzia eneo la Mto wa Mbu- Karatu Mjini hadi kwenye Geti la kuingia kwenye hifadhi ya Ngorongoro.

Dk. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa katika mipango yake ya kukuza Utalii Mkoani Arusha, Serikali atakayoiunda itaendelea na ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Ziwa Manyara Wilayani Karatu na uwanja wa ndege Waso uliopo Ngorongoro Mkoani Arusha.

Amesema Wilayani Karatu, takribani Shilingi Bilioni 88.5 kujenga kukarabati uwanja wa Lake Manyara kwa kuongeza barabara ya kurukia na kutua ndege pamoja na ujenzi wa jengo la abiria litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia watu 150 kwa wakati mmoja.

“Serikali yake itajenga barabara ya kuingia katika kiwanja hicho kwa kiwango cha lami ili kurahisisha shughuli za usafiri na Utalii kwa watalii watakaotumia uwanja huu,”amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here