Home MICHEZO Trionda mpira utakaotumika kombe la Dunia 2026

Trionda mpira utakaotumika kombe la Dunia 2026

Na Mwandishi wetu

SHIRIKISHO la Masoko Duniani (FIFA), limezindua mpira utakaotumika katika Michuano ya Kombe la Dunia 2026 uliopewa jina la Trionda ambapo una teknolojia maalumu.

Mpira huo unaitwa ‘Trionda’ -neno la Kihispania linalomaanisha mawimbi matatu ikiwa ni ishara kwamba Kombe la Dunia litaandaliwa na nchi tatu.

Mpira huo una rangi tatu, nyekundu, Kijani na Bluu, zikiwakilisha nchi tatu zitakazoandaa Kombe la Dunia 2026, Canada, Mexico na Marekani.

Pia kuna Nyota inayowakilisha Marekani, Lotus inayowakilisha Canada na Mamba anayewakilisha Mexico.

Mpira huo una teknolojia maalum ambayo itatuma taarifa kwa haraka kwenye VAR, ambayo itasaidia kugundua iwapo kuna faulo na itakuwa na uwezo wa kutambua aliyeugusa kwa mkono au katika kumtambua mchezaji mwingine aliyekosea.

Rais wa FIFA Gianni Infatino alisema amefurahishwa kuzindua Trionda unaoashiria umoja na mshikamano kwa waandaji wa Kombe la Dunia la 2026.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here