Na Mwandishi wetu ,Dar es salaam
TAKWIMU zinaonyesha asilimia 83 ya Wananchi walioshiriki kura ya maoni kutoka Mikoa 19 wamethibitisha kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29,2025 kwa kupiga kura.

Takwimu hizo zimetolewa na Kituo cha Sera za Kimataifa-Afrika(Centre for International Policy -Afrika CIP-Africa) ambapo kuanzia Septemba, 30 hadi Oktoba 5,2025 waliendesha zoezi kura za maoni Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani ili kupata twaswira ya hisia za Wananchi Kuhusu Hali ya kisiasa na mwelekeo wa Uchaguzi wa nafasi za wagombea Kupitia vyama vyao.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Oktoba 22,2025 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Tafiti na Uchapishaji wa CIP, Thabit Mlangi amesema wamefanya zoezi la kukusanya Kura za maoni kutoka katika Mikoa 19 Tanzania Bara huku Zanzibari Ikiwa miwili Pemba na Unguja ambapo Jumla ya waliohojiwa ni 1,976, wanawake walikuwa 988 na wanaume 988 Kati ya 1,976 waliohojiwa
“Asilimia 29 walikuwa na umri kati ya miaka 18 hadi 25, asilimia 32 wa umri wa miaka 26 hadi 35, asilimia 13 wa umri wa miaka 35 hadi 45, asilimia 17 wa umri kati ya miaka 45 hadi 55 na asilimia tisa (9) miaka 55 na kuendelea. Takwimu za kiwango cha elimu 4 zinaonyesha asilimia 14 walikuwa wenye elimu ya msingi; asilimia 57walikuwa na elimu ya sekondari; asilimia 28 walikuwa na elimu ya chuo; na,asilimia 1 walikuwa na elimu nyingine,” amesema.
Pia amebainisha kuwa katika sula la Mwelekeo wa siasa asilimia 81 ya walioshiriki
walijipambanua kuwa ni wafuatiliaji wa michakoya kisiasa nchini na asilimia 19 hawakuwa wafuatiliaji wa michako yakisiasa Kati ya wafuatiliaji wa michakato ya siasa, asilimia 43 walikuwa wanawake na asilimia 57 ni wanaume na katika kundi la wafuatiliajiasilimia 19 ni watu wenye elimu ya msingi, 55 wenye elimu ya sekondari,
asilimia 26 walikuwa wenye elimu ya chuo.
Hata hivyo akizungumza kuhusu ushiriki katika mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa kuelekea uchaguzi mkuu wa uraisi, ubunge na udiwani, asilimia 53 ya walioshiriki utafiti wameshiriki katika mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa kati ya waliohudhuria kwenye mikutano ya kampeni, asilimia 76 walihudhuria mikutano ya kampeni ya CCM, asilimia 2 walishiriki mikutano ya kampeni ya CHAUMMA, asilimia 15 wameshiriki mikutano ya kampeni ya ACT-Wazalendo asilimia 7 wameshiriki katika mikutano ya kampeni ya
chama zaidi ya kimoja.
“Matokeo ya utafiti yanaashiria kuwa asilimia 46 ya walioshiriki kura yamaoni wameonyesha kushawishiwa na sera za vyama vya siasa, ambapo
asilimia 54 wameonyesha kutoshawishiwa na sera za vyama,”amesema.
Amesema kura ya maoni ya urais ikiwa Uchaguzi Mkuu utafanyika hivi sasa, asilimia 84.5 ya walioshiriki kuraya maoni wameonyesha kuwa watampigia kura mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) huku asilimia 8 walibainisha kuwa kura yao ni siri yao asilimia 3 watampigia mgombea wa Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA) asilimia 3 watampigia mgombea wa Chama cha Wananchi
(CUF) na asilimia 1.5, National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi).
Aidha, kuhusu vipaumbele ambavyo wananchi wangependa wabunge namadiwani wao wavishughulikie baada ya Uchaguzi Mkuu ni kama pamoja ikiwemo,.Barabara (75%),Maji (75%)
Kuondoa michango mashuleni (61%)
Madawa kwenye zahanati(59%)
Pia Uendeshaji wa Uchaguzi Mkuu 2025
Asilimia 91 ya walioshiriki kura ya maoni wameonyesha kuridhishwa na jinsi Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) inavyosimamia zoezi la uchaguzi hadi sasa.