Home KITAIFA NCCR Mageuzi chawasisitiza watanzania kilinda amani ya Tanzania

NCCR Mageuzi chawasisitiza watanzania kilinda amani ya Tanzania

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

CHAMA Cha NCCR Mageuzi, kimewasisitiza Wananchi kudumisha amani na mshikamano na kuachana na baadhi ya watu wanaochochea vurugu hususani katika siku ya uchaguzi Mkuu Oktoba 29 Mwaka huu.

Wito huo umetolewa leo Oktoba 27,2025 na Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye pia ni Mgombea mweza wa urais kupitia Chama hicho Dkt.Evaline Wilbard Munisi wakati akizungumza na Waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.

“Tukio la kuchagua viongozi wa taifa kwa uchaguzi ni muhimu sana kwa maslahi ya watanzania wote hivyo isiwe upenyo kwa baadhi ya watu kutaka kuleta vurugu tuwakatae Kwa nguvu zote.

Amani na utulivu iliyopo si kwa bahati mbaya kwa watanzania bali ni kwa mapenzi ya Mungu, hivyo ni utajiri mkubwa tulionao kuliko madini yalipo, kila Mtanzania ana wajibu wa kuilinda isiyoweke,”

“Ndugu Wanahabari Amani na Mshikamano katika Taifa lolote ni utajiri mkubwa kuliko dhahabu,almasi,Vito na kadhalika,hivyo kila Mtanzania anayo dhamana kubwa ya kuvilinda vitu hivyo kwa gharama yoyote ile bila kujali itikadi zetu za dini na kisiasa.”Amesema Dkt.Munisi

Aidha amesema kuwa tangu vyama vya siasa vianze kampeni za uchaguzi haijatokea shida yoyote juu ya uendeshaji wa kampeni hizo,hali ambayo inatokana na amani nammshikamano uliopo nchini,nakwamba utulivu huo haupo kwa bahati mbaya bali unatokana na misingi bora ambayo imewekwa na viongozi wa kisiasa  na wanaosimamia uchaguzi wenyewe ikiwemo Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC).

Aidha amesema kuwa katika Ilani ya chama hicho ya mwaka 2025 moja ya ajenda zake ni “Muafaka wa Kitaifa”ambapo wanaamini kuwa misingi ya amani na mshikamano ni muafaka wa Kitaifa kwa kuwa na maridhiano ya pamoja na kujenga Taifa.

“Tutapata haki na usawa kama ilivyokua kwenye kubadili baadhi ya Sheria na kanuni za uchaguzi kwa pamoja,vyama vya siasa vilishikamana na kupendekeza marekebisho madogo naya msingi kuelekea uchaguzi Mkuu 2025 kwa kuwa Serikali ni sikivu ikayazingatia,matokeo yake tunaendesha kampeni zetu kwa amani ” amesema Dk.Munisi.

Nakuongeza” katika kuthibitisha hilo hadi sasa hatujashuhudia pingamizi lolote,hatua hii inatupa imani kama chama kuwa haki itatendeka na kila atakayeshinda atatangazwa,kwa jambo hili tunaipongeza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi chini ya Mkurugenzi wake ndugu Ramadhan Kailima.”

Aidha amehitimisha kwa kusema kuwa NCCR-Mageuzi kama kilivyoamua kwa ridhaa yake kushiriki uchaguzi mkuu basi hakitamani wala hakitaki kuona uchaguzi ukivurugika wala vichocheo vyovyote vya kuleta taharuki na hofu kwa wapiga kura wake siku ya uchaguzi.

“Tunapinga maandamano ya aina yoyote ile isipokua maandamano yetu mtayaona kwenye masanduku ya kupigia kura kwani tutajitokeza kwa wingi ili kupiga kura kusudi tukalete mabadiliko na Mageuzi ambayo sote tunayataka”.amesema 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here