Home KITAIFA Mkutano wa Kimataifa wadau wa kilimo cha mboga na matunda kufanyika nchini

Mkutano wa Kimataifa wadau wa kilimo cha mboga na matunda kufanyika nchini

Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

ASASI ya Kilele Sekta Binafsi inayoendeleza na kukuza Sekta ya Horticulture nchini (TAHA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo imeandaa mkutano mkubwa wa wadau wa mazao ya mboga na matunda utakaowakutanisha washiriki kutoka ndani na nje ya nchi, kwa lengo la kujadili fursa, changamoto na mikakati ya kukuza Sekta hiyo.

Mkutano huo utafanyika tarehe 12 – 13 Novemba 2025 jijini Dar es Salaam, ukiwa ni wa kwanza wa aina yake nchini, na utaendelea kufanyika kila mwaka.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli, Amesema hayo Novemba,6 2025 wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari, jijini Dodoma na kueleza kuwa wadau watapata fursa za kujadili sera, teknolojia, fursa za masoko, pamoja na miundombinu inayohitajika ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya mboga na matunda.

Amesema kuwa mkutano utahudhuriwa na wadau zaidi ya 400 na kuwa chachu ya kukuza ushirikiano kati ya Serikali, Sekta Binafsi na Wadau wa Maendeleo katika kuboresha kilimo cha mboga na matunda.

Amefafanua kuwa zaidi sekta ya mboga na matunda imeendelea kuwa chanzo muhimu cha mapato kwa wakulima na Taifa kwa ujumla, kutokana na mchango wake katika Pato la Taifa na upatikanaji wa fedha za kigeni.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Asasi Kilele ya Sekta Binafsi inayoendeleza na kukuza Sekta ya Horticulture nchini (TAHA), Dk. Jacqueline Nkindi, amesema mkutano utawajenge wakulima uwezo wa kutumia teknolojia za kisasa na kuwafungulia masoko mapya ya kimataifa.

Amebainisha kuwa TAHA imejiwekea malengo ya kuongeza thamani ya uzalishaji wa mazao hayo kwa takribani Dola za Kimarekani bilioni mbili kufikia mwaka 2030 hadi 2035.

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), Irene Mlola, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwekeza kwenye Sekta ya Kilimo, akisema hatua hiyo imeongeza tija na ushindani katika uzalishaji wa mazao ya bustani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here