Home KITAIFA Tutaunda  Wizara kamili ya vijana-Rais Samia

Tutaunda  Wizara kamili ya vijana-Rais Samia

Na Esther Mnyika,  Dodoma 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan ameliambia Bunge la Tanzania  kuwa anadhamiria kuunda Wizara kamili ya Vijana badala ya kuwa na idara ndogo ndani ya Wizara yenye kushughulikia masuala ya Vijana.

Dk. Samia amebainisha hayo leo Novemba 14, 2025 Bungeni jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Bunge la 13 la Tanzania, akieleza kwamba anafikiria pia kuwa na washauri wa masuala ya Vijana ndani ya Ofisi ya Rais, Ikulu.

“Kwa kuwa zaidi ya asilimia 60 ya watu wa nchi hii ni Vijana, tutaweka kipaumbele pia kwenye sera na programu zitakazipanua fursa za kiuchumi, kutengeneza kazi na ajira na kukuza wigo wa hifadhi ya jamii na kuwajengea kesho iliyobora ili Vijana wapate nafasi ya kushiriki kujenga mustakabali mwema wa Taifa letu,” amesema Dk. Samia.

Dk. Samia pia ameahidu kuweka msisitizo katika masuala ya Vijana, akisema anatambua uwepo wa majukwaa mengi ya kuwafikia vijana ila bado shughuli zao zinafifishwa na masuala ya kisiasa, akiahidi kuchukua hatua za kuongeza mitaji za shughuli za kiuchumi kwa kutenga shilingi bilioni 200.

Ameahidi pia kuanzisha madirisha ya uwekezaji kwa vijana ili kutoa mikopo na mitaji nafuu ya biashara za Vijana, akisema ni dhima ya serikali kuendeleza ukuaji wa uchumi wakilenga kujenga kujenga Taifa jumuishi lenye ustawi, haki na lenye kujitegemea ikiwemo kuwekeza zaidi katika sekta za Kilimo, uvuvi, viwanda, utalii na ujenzi ili kukuza uchumi kufikia zaidi ya asilimia 7 kufikia mwaka 2030.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here