Home KITAIFA Mbeto awatahadharisha Viongozi wa Dini awaomba watoe ushauri bali wasijiingize katika Siasa

Mbeto awatahadharisha Viongozi wa Dini awaomba watoe ushauri bali wasijiingize katika Siasa

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)kimewaasa Viongozi wa Dini kuacha kuvaa viatu vya kisiasa kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kulipoteza Taifa katika dira na ramani yake ya Umoja, Udugu na Amani.

Pia chama hicho kimesema uamuzi wowote wa Viongozi hao kuingilia siasa si katika jambo lenye muafaka kwa nyakati zote.

Katibu wa Kamati Maalum vya NEC Zanzibar , Idara ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo, Khamisi Mbeto Khamis ,ameeleza hayo katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Visiwani humu .

Amesema matatizo yaliochomoza yana taaswira yac Siasa hivyo ni busara utatuzi wake , ukachwaa mikononi mwa Serikali na wanasiasa huku viongozi wa Dini wakisubiri kushirikishwa itakapohitajika .

Amrsema hata inapozuka mizozo au mitafaruku ya Kidini Makanisani kwenye Mahekalu na Misikitini ,Wanasiasa hawana nafasi ya kushiriki katika kufikia utatuzi , ni busara pia kwa viongozi wa Dini kutoingilia Siasa.

“Viongozi wa Serikali hawajachoka kutafuta Suluhu na utatuzi kwa yaliotokeea. Si vyema na wala si ustaarabu Viongozi wa Dini kuwapangia hatma viongozi Serikali lipi la kufanya,”amesema Mbeto .

Akizumgumza kwa utulivu, Katibu huyo Mwenezi , alisema inasikitisha kuona Viongozi wa Dini Kuu , Uislam na Ukristo, wakianza kuzungumzia masuala ya kisiasa ndani ya nyumba za ibada kwa jazba na hamaki .

‘Taifa linaoongozwa na Serikali ya Rais , Mkuu wa Nchi mwenye mamlaka kisheria na kikatiba. Hajashindwa kumaliza yaliojitokeza .Ikiwa viongozi wa Dini watahitajika wataitwa kutoa ushauri itakapobidi,”ameeleza.

Aidha amesema kwa namna yoyote ikiwa Viongozi wa Dini wataendelea kutoa matamko yenye hofu na taharuki katika jamii , Taifa linaweza kupitishwa katika Jangwa la hatari nyeusi isioepukika.

“Mwalimu Julius Nyerere amewahi kutamka hadharani Serikali ya Tanzania haina Dini. Wananchi ndiyo wenye imani za Dini .Hivyo si vyema baada ya miaka 60 Dini zijibebesha dhamana za kisiasa,” amefafanua Mbeto.

Ameongeza kuwaViongozi wa Dini wasiendelee kutoa matamko ya kuisakama Serikali kwani kwa kufanya hivyo, watakuwa hawajengi mustakabali chanya wa taifa letu.

“Inapozuka mivutano ya Dini huwa haina msalie wala sumile. Milipuko na varange zake huwa si kidogo kama inavyodhaniwa. Chonde jazba zisilipitishe Taifa katika bahari ya damu,”anesema

Mbeto amesema misuguano iliowahi kutokea nchini kati ya Serikali ya chama tawala na Upinzani, ilimalizika kwa njia ya mazungumzo mezani bila kupata shinikizo toka mahali popote .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here