Home KIMATAIFA Bodi ya Bima ya Amana yashiriki mkutano wa 24 wa mwaka...

Bodi ya Bima ya Amana yashiriki mkutano wa 24 wa mwaka wa taasisi za bima ya amana duniani nchini Ureno

Na Mwandishi wetu

BODI ya Bima ya Amana (DIB) inashiriki katika Mkutano Mkuu wa 24 wa Taasisi ya Kimataifa ya Bima za Amana (IADI) unaofanyika jijini Lisbon, Ureno kupokea na kujadili taarifa mbalimbali za kamati za kikanda za IADI pamoja na kikao cha 83 cha Baraza la Utendaji la IADI.

DIB inawakilishwa na Mkurugenzi Mkuu, Isack Kihwili, ambaye tayari amewasili jijini Lisbon tayari kwa mkutano huo unaoanza Novemba 24 hadi 28, 2025.

Kamati za kikanda za IADI zinazotarajiwa kukutana wakati wa mkutano huo. Hizo ni pamoja kamati za kanda ya Afrika ambako DIB iko, kanda za Asia Pasifiki, Eurasia, Mashariki ya Katika na Kaskazini mwa Afrika, Caribbean, Latini Amerika, Ulaya na Amerika Kaskazini.

Aidha, wakati wa mikutano hiyo, Kamati ya Wataalam ya Bima ya Amana ya Kiislamu pia inatarajiwa kukutana. Mikutano mingine itakayofanyika ni kuhusu masuala ya kisera, udhibiti wa ndani, mipango na utekelezaji za IADI.

IADI ni taasisi ya kimataifa ya bima za amana ambayo inaandaa viwango vya kimataifa vya mifumo ya bima ya amana na ni jukwaa kuu la taasisi za bima ya amana duniani kukutana na kubadilishana uzoefu na ujuzi.

Ilianzishwa mwaka 2002 na inasaidia mamlaka mbalimbali kuimarisha mifumo ya bima ya amana kwa kuongeza ufanisi wa kisera na viwango, kusimamia utekelezaji wake pamoja na kukusanya taarifa za bima za amana na kuanguka kwa benki.

IADI ni jukwaa linalotumika pia kubadilishana mbinu za mifumo yenye ufanisi ya bima ya amana, usimamizi na utatuzi/ufumbuzi wa migogoro ya benki.

Hadi sasa IADI bima za amana wanachama 107 kutoka duniani kote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here