Home MICHEZO Hasheem Thabit: Mchezo ulikuwa mgumu

Hasheem Thabit: Mchezo ulikuwa mgumu

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

NAHODHA wa Timu ya Basketball ya Dar City, Hasheem Thabit, amesema mashindano waliyoshiriki nchini Kenya yalikuwa na ushindani mkubwa, lakini wanashukuru kwa nafasi waliyoipata na matokeo waliyofikia.

Akizungumza mara baada ya kurejea nchini, Thabiti amesema mchezo wa basketball una siku zake, na si kila mara matokeo huwa upande mmoja.

“Basketball ni mchezo wa tofauti; si kila siku mchezo utakuwa wako. Kuna siku utaongoza, na kuna siku utapata changamoto. Wachezaji gani tunawahitaji, tunaweza kuendelea nao, na wapi wanauwezo mdogo hayo yote tunapaswa kuyapima,” amesema Thabiti.

Nahodha huyo ameendelea kusisitiza kuwa ameshinda michezo mingi ya basketball na anaifahamu vema namna mchezo unavyobadilika kulingana na mazingira na ubora wa timu pinzani.

Klabu ya Dar City ilishukuru Mungu kwa mafanikio waliyoyapata katika mashindano hayo, ikiwemo kushika nafasi ya tatu, ikiwa ni ishara ya uwakilishi mzuri kwa Tanzania.

Kwa upande wake, Kocha wa timu hiyo Mohamed Mbwana amesema wachezaji wamefanya kazi kubwa na kuonyesha kiwango kizuri katika mashindano hayo.

“Kikubwa ni kwamba tumefanikiwa kupeperusha bendera ya Tanzania. Watu wamekuwa wakiuliza, ‘Dar City ni timu gani?’ Hii inaonyesha tumekuwa mabalozi wazuri,” amesema Kocha.

Aidha, Kocha huyo alimsifu nahodha huyo akisema:“Zuzuwa, BL Hashimu Thabiti amefanya vizuri sana hasa katika kupambania na kupigania timu kwenye nafasi za juu.”Kocha alihitimisha kwa kusema kuwa uamuzi kuhusu wild card ya msimu wa 2025/2026 watakuwaacha viongozi wa ligi (BL) kuamua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here