Home KITAIFA Wateja  wa iliyokuwa Benki ya FBME kulipwa  asilimia  30 awamu ya tatuNa...

Wateja  wa iliyokuwa Benki ya FBME kulipwa  asilimia  30 awamu ya tatuNa Mwandishi wetu

Na Mwandishi wetu

BODI ya  Bima ya Amana (DIB)  ipo katika mchakato wa kulipa fidia ya ufilisi awamu ya tatu ya asilimia 30 kwa  wadaiwa iliyokuwa Benki ya FBME walioko Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo Disemba, 1 2025 na Bodi  hiyo imesema  malipo  hayo yanafanya wadai FBME  nchini wawe wamelipwa jumla ya asilimia 85 ya madai yao kwani katika awamu  ya kwanza na ya pili walilipwa asilimia  30 na asilimia 25 mtawalia.

“Kutokana na tathmini iliyofanywa, DIB imeamua kulipa fidia ya ufilisi kwa wadai waliokuwa na amana zaidi ya shilingi milioni 1,500,000.00 katika benki ya FBME kwa awamu ya tatu kwa upande wa wadaiwa Tanzania pekee,’’ amesema Mkurugenzi Mkuu wa DIB, Isack Kihwili katika taarifa yake.

AidhaKamati ya Wadai imeshaidhinisha pendekezo la malipo hayo.Kwa ujumla, wadai kwa upande wa Tanzania ni 1,414, ambao madai yao ya jumla kwa benki hiyo ni shilingi bilioni 35.2; wadai wa kimataifa (TIB) wako 866 na madai yao ni shilingi bilioni 308.22. 

Aidha,wateja wa tawi la Cyprus ni 5,480 wakidai jumla ya Euro milioni 1,254.62 (sawa na shilingi milioni3,596.00).

‘’Malipo ya awamu nyingine yatategemea kiasi kitakachokusanywa ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa fedha zilizozuiliwa na mamlaka ya Marekani (FinCEN),’’ ameeleza Mkurugenzi Mkuu wa DIB na kuongeza kuwa kuzuiliwa kwa fedha hizo ni moja ya sababu kubwa zilizochelewesha mchakato wa malipo ya fidia ya ufilisi.

Aidha, DIB kama mfilisi, itaendelea kufanya tathmini kadiri makusanyo yatakavyopatikana na kufanya malipo ya awamu nyingine kwa wadai pindi yatakapokuwa ya kuridhisha.

Benki Kuu ya Tanzania ilifuta leseni ya Benki ya FBME mwaka 2017 kutokana na kukiuka masharti ya leseni yake na kuichagua DIB kama Mfilisi. FBME ilikuwa na makao makuu yake hapa nchini na tawinchini Cyprus. Hiyo imefanya zoezi la ufilisi kushirikisha mamlaka za Tanzania na Cyprus.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here