Home KITAIFA Oryx Gas Yakabidhi Zawadi kwa Washindi wa Kampeni ya “Gesi Yente”

Oryx Gas Yakabidhi Zawadi kwa Washindi wa Kampeni ya “Gesi Yente”

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imewahakikishia Watanzania kuwa itaendelea kuboresha huduma zake kwa kuboresha miundombinu, kupanua mtandao wa usambazaji, ili kutekeleza ajenda ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa ajili ya afya bora, mazingira safi, na maendeleo endelevu.

Akizungumza leo Desemba 1,2025 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa wateja walioshinda zawadi mbalimbali za kampeni ya GESI YENTE yenye lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia,Meneja Maasoko na Mauzo wa kampuni hiyo Shaban Fundi amesema kampuni hiyo imeendelea kuhimiza matumizi ya nishati hiyo.

“Kama Tanzania kuna malengo ambayo yamewekwa asilimia 80 wawe wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034 na sisi kama Oryx hatuko nyuma katika hilo tumeweza kuweka mkakati kuhakikisha huduma
zetu zinawafikia wananchi wa maeneo yote kupitia mawakala wetu wakubwa na wadogo.

“ Na katika kampeni ya GESI YENTE wateja zaidi ya milioni moja wameshiriki kwa kutuma jumbe kupitia kadi ambazo tumeweka katika mitungi yetu na ushiriki huo unamaana kubwa kwetu kwa maana wateja wetu wanatuamini kutokana na ubora wa gesi pamoja na huduma zetu kuwa za uhakika.”

Amesema kupitia kampeni hiyo wanajivunia wateja wao huku akitoa rai kwa wananchi wasidanganyike kwa kubadilishiwa mitungi kwani kuna baadhi ya mawakala wasiowaaminifu wanawashawishi wateja wa Oryx wanawabadilishia mitungi.

“Ukishautoa mtungi wako wa Oryx haitakuwa rahisi kuupata mtungi mwingine.Hivyo ni vema wakahakikishia mtungi wako wa Oryx unabakia nao mwenyewe.”

Kuhusu kampeni ya GESI YENTE amesema kampeni hiyo ilianza Agosti 13 mwaka huu wa 2025 na ilikuwa ya miezi mitatu lakini kutokana na maombi ya mawakala kuwa iendelee hivyo wameisogeza mbele hadi Desemba 15 mwaka huu,hivyo ametoa rai kwa wateja kuendelea kushiriki ili kujishindia zawadi mbalimbali.

“Tangu tulipozindua kampeni hii ya GESI YENTE yenye lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia mwitikio mkubwa umekuwa mkubwa sana,tumefikia wateja wengi,tumeshuhudia wateja wa Oryx wakituma jumbe mbalimbali kupitia maelezo tuliyoweka katika kadi zilizipo katika mitungi yetu ya gesi.”

Amesisitiza ni zaidi ya watu milioni moja wameshiriki kampeni hiyo kwa wamekwangua kadi na kutuma ujumbe na ndio maana kampuni hiyo imeamua kuongeza muda wa kampeni hii ambayo sasa itamalizika Desemba 15 mwaka huu.

Kwa upande wa wateja ambao wameshinda zawadi za majiko ya Oryx,baiskeli ,pikipiki na mabegi ya shule wameipongeza kampuni hiyo kwa kuwa na kampeni maalum yenye lengo la kuhamasisha jamii ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa.

Irene Godfrey ambaye ni mkazi wa Mbezi Beach Dar es Salaam aliyeshinda zawadi ya pikipiki amesema kampeni ya GESI YENTE imemuwezesha kumpatia mtaji kwani pikipiki hiyo ataitumia kwa shughuli mbalimbali za uzalishahi huku akisisitiza matumizi ya gesi ya kupikia ndio mkombozi wa afya na mazingira.

Kwa upande wake Elikana Madirisha amesema kuwa kupata jiko la Oryx kwake inakwenda kurahisisha katika kuandaa chakula kwani kupiga kwa gesi kunarahisisha muda wa kukaa jikoni na muda mwingi kutumika katika kufanya maendeleo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here