Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
RAIS Dk Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa dini kuacha kujivika majoho ya kuendesha nchi kwa utashi wao binafsi, bali Tanzania itaongozwa kwa Katiba.

Ameeleza kuwa Tanzania haitendeshwa kwa madhehebu ya dini bali kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Dk Samia ameeleza hayo leo, Disemba 2, 2025 akihutubia Taifa katika mkutano wa Rais Samia Suluhu Hassan na wazee wa Jiji la Dar es Salaam.
“Ubora wa dini upo mioyoni mwetu, hakuna overriding hapa…Kwamba mimi dini yangu, nitaoveriding Tanzania, nikilitoa ndio hilohilo…,”

“Toka nimekaa matamko nane yametolewa na TEC, lakini ukienda chini wenyewe kwa wenyewe wanapingana, matamko hayafanyi kazi vizuri,”
Amesema Tanzania ni nchi ya umoja, mshikamano ndio ngao, akiwataka Watanzania kutokubali kuvurugana kwa misingi ya dini na kisiasa, hata kama aliyeopo madarakani haumpendi.
“Kama haumpendi anayeongoza mvumilie tu…mioyo yote imeumbwa”



