Home KIMATAIFA Waziri Kombo na Profesa Kabudi wafanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa...

Waziri Kombo na Profesa Kabudi wafanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Misri

Na Mwandishi wetu, Misri

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi wamekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Misri ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Viwanda na Uchukuzi Mhe. Kamel Al-Wazir Disemba 18, 2025 katika Ofisi zake zilizopo kwenye Mji wa Utawala Jijini Cairo nchini Misri.

Katika Mazungumzo yao, Mawaziri hao wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali yakiwemo Uchukuzi, Kilimo pamoja na Viwanda.

Pamoja na ushirikiano mzuri uliopo kati ya mataifa haya mawili, Balozi Kombo amemhakikishia Mhe. Naibu Waziri Mkuu Kamel kuendelea kushirikiana na Misri katika Nyanja mbalimbali kwa manufaa ya mataifa yote mawili.

Aidha, kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu Kamel, amemueleza Kombo juu ya nia ya Misri kujenga viwanda vikubwa katika eneo lililopo Kwala Mkoani Pwani, kutokana na sera nzuri za uwekezaji pamoja na maendeleo ya kuimarisha miundombinu thabiti ya kuwezesha kuwekeza katika mazingira mazuri na ya uhakika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here