Na Esther Mnyika, Dar es Salaam
BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA ) limetangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Darasa la Nne ambapo ufaulu umepanda kwa asilimia 2.67 na asilimia 88 ya wanafunzi wamefaulu kidato cha pili.

Jumla ya wanafunzi 1,493,377 walisajiliwa kufanya mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la nne na kwa mtihani wa kidato cha pili jumla ya wanafunzi 898718 walisajiliwa kufanya mtihani wa upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili.
Akitangaza matokeo hayo leo Januari , 10 2025 jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohamed amesema Jumla ya wanafunzi 1,583,686 waliosajiliwa kufanya mtihani wa upimaji wa darasa la nne wakiwemo wasichana 818,673 sawa na asilimia 52 na wavulana 765, 013 sawa na asilimia 48.
“Mahudhurio ya wanafunzi wa darasa la nne yalikua asilimia 94 sawa na wanafunzi 1, 490, 377 katika shule za msingi 20, 508 ambapo ufaulu kwa wasichana wamefaulu kwa asilimia 53 huku wavulana ikiwa asilimia 47,”amesema.
Amesema wapo wanafunzi 93, 309 sawa na asilimia 6 hawakufanya mtihani huo pamoja kuwa walisajiliwa.
Pia Baraza limefutia matokeo ya wanafunzi 41 waliofanya udanganyifu na 8 walioandika matusi kwenye majibu yao katika upimaji kitaifa wa darasa la nne.
Profesa Mohamed akizungumzia mtihani wa upimaji kidato cha pili amesema Jumla ya wanafunzi 898,718 walisajiliwa wakiwemo wasichana 497, 891 sawa na asilimia 55.48 na wavulana 400,827 sawa na asilimia 44.5.
Ameongeza kuwa waliofanya mtihani huo walikuwa wanafunzi 811,575 sawa na asilimia 91.3 katika shule za sekondari 6,223 na wanafunzi 77,689 sawa na asilimia 8.7 hawakufanya upimaji wa mtihani huo na pamoja kuwa walisajiliwa.
Amesema Baraza hilo limefuta matokeo ya wanafunzi 29 waliofanya udanganyifu na 11 walioandika matusi katik upimaji wa kitaifa kidato cha pili.
Profesa Mohamed amesema baraza hilo limeweka wazi kuwa litawafuatilia wanafunzi 19 walioandika matusi kwenye mtihani wa umipimaji kitafa darasa la nne na kidato cha pili uliofanyika 2025 kuhakikisga shule zinawachukulia hatua.
Amesema ufuatiliaji huo utafanyika kwa kuandika barua kwa wakuu wa shule husika za wanafunzi hao kuwa bado wako kwenye mfumo wa shule husika za wanafunzi hao pia wataandika barua kwa mamlaka zao ikiwemo wakuu wa shule na bodi za shule au kamati za shule kwa ngazi ya shule ya msingi ikiwahusisha wazazi kuchukua hatua ili kuhakikisha suala la kuandika matusi linakomeshwa kabisa.



