Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
VIJANA na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam wamesema wanatambua na kuthamini mchango wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuwekeza kwenye maarifa kwa ajili ya vijana, kufungua fursa mbalimbali za maendeleo, na kulinda maslahi ya Taifa kwa ujumla.

Ikiwa leo Januari, 27 2026 ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwakwa kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan vijana hao wameungana kumuonesha upendo katika siku yake ya kuzaliwa Rais Samia wamesema wameridhishwa na uongozi wake unaowekeza na kuzalisha fursa kwa vijana.
Akizugumza leo Januari, 27 2026 jijini Dar es Salaam kwenye hafla Mratibu wa Taasisi ya Together For Samia, Gulatone Masiga, ambaye ni mmoja wa waandaaji wa hafla hiyo, amesema lengo la mkusanyiko huo ni kuwakutanisha vijana wa kizazi kipya pamoja na wananchi wenye mapenzi mema kwa Taifa ili kumuonesha Rais heshima na shukrani.

“Hii si sherehe tu, bali ni ishara kwamba vijana wa kizazi kipya na wananchi wenye mapenzi mema kwa Taifa tunatambua uongozi unaotujali na kutupa nafasi. Tumeona ni vyema kuandaa shughuli ya kuwakutanisha ili kuonesha upendo na heshima kwa Rais ambaye ni mlezi wa vijana na maendeleo ya Taifa,” amesema.
Amesema Rais Dkt. Samia ni kiongozi anayefungua milango ya fursa kwa vijana, mlezi wa ndoto zao na anayesikiliza mawazo ya kizazi kipya huku akisimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa usawa kote nchini.
Amesema vijana walioshiriki katika hafla hiyo ni wa kizazi kipya ambao wamenufaika kwa kiasi kikubwa na uongozi wa Rais Dkt. Samia katika takribani miaka mitano ya uongozi wake.

Ameeleza kuwa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, Masiga alitaja ujenzi wa vyuo vya ufundi na ujuzi katika wilaya zaidi ya 62 nchini, hatua iliyowezesha vijana wengi kupata maarifa na stadi za kujiajiri.
Pia amesema Serikali imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu kwa kuanzisha mtaala mpya unaolenga kuhakikisha wahitimu wa elimu ya msingi na sekondari wanapata maarifa na vyeti vinavyowawezesha kujiajiri.
Kwa upande wake, kijana mzalendo Dorcas Mshiu amesema kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, vijana wengi wameanza kusajili biashara zao, hali inayoonesha kuwa mazingira ya biashara yamefunguka.

“Nasimama kifua mbele kusherehekea siku hiyo maalumu ya Rais Dkt. Samia kwasababu Rais huyo amekuwa mama anayewakumbuka vijana na kuwafungulia fursa mbalimbali ndani ya nchina nje ya nchi, ” amesema
Dorcas amesema vijana wanaojiajiri wamenufaika na mkakati maalumu wa mikopo yenye riba ya asilimia nne, unaowawezesha kuanzisha na kuendeleza biashara zao naamefungua milango ya uwekezaji, hali iliyoongeza ajira kwa vijana wengi nchini
“Rais Dk.Samia amefanya mabadiliko mbalimbali katika sekta za i afya, nishati, elimu na zinginezo na amekuwa na kipaumbele cha maridhiano na amani hivyo vijana tumpenda na tupo pamoja nae,” ameongeza.



